Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Diamond Platnum. Show all posts
Showing posts with label Diamond Platnum. Show all posts

Alichosema Meneja wa Diamond Kuhusu Kufanya Kolabo na Kanye West Hiki Hapa

Siku chache baada ya msanii Diamond platnumz kupost picha kwenye instagram akiwa na kanye West ambaye ni rapper mashuhuri ulimwenguni watu wengi wamekuwa wakihisi pengine kuna kolabo inaweza kutokea hasa baada ya kusemekana wasanii hao walibadilishana namba.

akihojiwa na redio moja mmnoja wa mameneja wa Diamond,Sallam amesema kuwa huwezi kufanya kolabo na msanii kama kanye West kisa umekutana naye tu kwani kuna protokali nyingi zinabidi zifuatwe mpaka kukamilisha hilo na kuongeza kuwa kwa CV ya Diamond nafasi inaweza kupatikana.

“Unajua wenzetu hawafanyi kolabo kwa sababu umekutana naye,lazima utengeneze kuwa wewe ni nani,ukifanya naye kolabo itamsaidia nini yeye,nashukuru kwa upande wetu tuna Cv nyingi kwa hiyo nadhani itatusaidia kwa upande mwingine” alifunguka Sallam.
3

Picha za Shoo ya Diamond Platnumz Alivyowasha Moto Kwenye Concert Nchini Uganda..Zari Naye Alikuwepo

Usiku wa jana msanii Diamond Platinum alitumbuiza kwenye tamsasha kubwa ‘Born 2 Win Concert’ jijIni Kampala, Uganda.
Mbali na Diamond msanii Patoranking naye alitumbuiza kwenye tamasha hilo.

Hizi ni baadhi ya picha za Diamond akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
DIAMOND13
Diamond1341DIAMOND134DIAMOND288DIAMOND186
3

Diamond Platnumz Aikacha Party ya Zari All White Ciroc Party, Ex wa Zari na Wapambe Wake Wahuzuria, Picha Hizi Hapa

Wana watoto watatu pamoja na wana biashara kibao za pamoja, hivyo ni ngumu kwa Zari na mume wake wake wa zamani, Ivan kupotezeana licha ya kila mmoja kuchukua njia yake kimahusiano.

Ivan na jamaa zake wa Rich Gang wakila bata kwenye Zari All White Party

Ndio maana Ivan na mpambe wake King Lawrenc walisafiri kutoka SA na kwenda kumuunga mkono Zari ambaye Alhamis hii aliandaa party yake ya kila mwaka ya mavazi meupe tu kwenye kiota cha Guvnor kilichopo Kampala Uganda.

Zari All White Ciroc Party
Zari All White Ciroc Party

ZARI8912ZARI834ZARI234ZARI734


ZARI0923


ZARI13

ZARI90

TOA 3

Photos: Mama Zari Visits Diamond And Zari In Dar To See Granddaughter Tiffah Dangote.

Zari
Mama Zari flew from Uganda to Tanzania this weekend to see her granddaughter Tiffah Platnumz Dangote who was born 3 weeks ago, And do you see the stunning home of Diamond and Zari ...!


3

Madai Mtoto si wa Diamond, Zari Aitwa Kwao Uganda

KIMENUKA! Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan ‘Zari’ (mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni, Zari alipigiwa simu na mama yake mzazi, Halima Hassan akimtaka aende nyumbani kwao ili akawaeleze ukweli ndugu zake ambao wamekuwa njia panda baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Tiffah si wa Diamond ambaye familia inamtambua kwa sasa.
“Taarifa zinawafikia tofauti. Kuna zile za awali kwamba mtoto huyo ni wa Ivan, mara zikaibuka nyingine kwamba ni wa King Lawrence hivyo mama amemuita Zari ili akategue kitendawili hicho kumaliza ubishi.

ATAKIWA KWENDA NA UKWELI
“Amemtaka aende na ukweli moyoni maana yeye (Zari) ndiye anayeujua. Hata hiyo DNA haina maana. Ameambiwa kwamba siku zote mama ndiye anayejua ukweli wa mtoto ni wa nani,” kilisema chanzo hicho.

ATAKIWA AMUOGOPE MUNGU
Chanzo kilizidi kunyetisha kuwa, mbali na kumtaka aende na ukweli, familia imemtahadharisha atakapofika aseme ukweli kwa kumuogopa Mungu maana vinginevyo dhambi hiyo itamhukumu maisha yake yote.
“Ametahadharishwa na familia kwamba anapaswa kumuogopa Mungu maana ni dhambi mtoto wa baba huyu kumpa baba huyu. Wao Kama familia wanajua Tiffah ni wa Diamond. Sasa wanakangaywa na hao wanaodai wao ndiyo haswa wahusika.

HAWAHOFII KAMA SI WA DIAMOND
“Familia imesema haina shida hata kama itakuwa mtoto si wa Diamond lakini wanachotaka wao ni kujua ukweli tu.” Chanzo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya King Lawrence kuibuka na barua ya wakili kuitisha kipimo cha DNA akidai mtoto ni wake, Diamond alisisitiza kwamba mtoto huyo ni damu yake hivyo hana muda wa kubishana na mtu.

“Huyo jamaa (King Lawrence) atakuwa anatafuta kiki katika vyombo vya habari. Huyohuyo ndiye alianza kusema mtoto si wangu ni wa Ivan mara amegeuka tena na kusema ni wake yeye, hata haeleweki. Siwezi kujibishana naye.
“Hata hiyo barua aliyosema ni ya wakili ya kutaka DNA, haijatufikia! Nasikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alisema Diamond.

KUHUSU SAFARI
Alipotafutwa Diamond ili aeleze kuhusu taarifa za mama Tiffah kuitwa nchini Uganda ili akaeleze ukweli, alisema hayo ni mambo ya kifamilia zaidi na hata hivyo haoni tatizo ndugu kumwita Zari kwani ukweli Tiffah ni damu yake na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea.
“Tiffah ni damu yangu hata akienda hakuna kitakachobadilika. Sina wasiwasi maana mimi najua mahesabu yake yote na ninajua mpaka tarehe niliyokutana naye na mtoto akawepo,” alisema Diamond huku akisema, Zari hana nafasi ya kuongea na vyombo vya habari.

NCHINI UGANDA
Nchini Uganda, bado baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mkanganyiko wa mtoto wa Diamond ambapo baadhi ya magazeti yametaka Zari aende akapime DNA ili kujiridhisha kuhusu uhalisia.

AFRIKA KUSINI
Nazo habari kutoka nchini Afrika Kusini ambako ndiko kwenye makazi ya Zari, baadhi ya Wabongo wanaoishi jirani na Zari walisema wanatambua uwepo wa Diamond kama mpenzi mpya wa Zari kwa hiyo hakuna shaka kuwa yeye ndiye baba (biological father) wa Tiffah.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu juzi, mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Steve, alisema amekuwa akimfuatilia kwa karibu King Lawrence kupitia Instagram yake akidai kwamba yeye ni baba wa Tiffah, lakini sehemu kubwa ya watu wenye ujirani na Zari kule wanaamini, Diamond ndiye baba husika.

“Kuhusu Diamond kuwa baba wa Latifah hilo halina ubishi. Hata sisi huku tunajua hivyo. Hili suala liangaliwe kwa macho matatu. Nahisi kuna ‘vita’ ya sisi Watanzania na Waganda kuhusu mtoto,” alisema Mbongo huyo.

Source:Globalpublishers 3

Haya Ndio Majibu ya Diamond Platnumz Kuhusu ishu ya Mtoto Kupimwa DNA…

Kumekuwa na stori ambayo imechukua sana headlines kuanzia mitandaoni mpaka kwenye Magazeti inayomhusu Diamond, Zari na mtoto wao.

Diamond amepatikana na kutolea majibu ishu hiyo, barua ya kudai mtoto wake akapimwe DNA bado haijamfikia na kama ni ishu ya Kisheria inayohusu Mahakama amesema ingepitia kwa Wakili au Mwanasheria na sio kupitia Mitandaoni.

Kingine amesema kwamba Zari hajawahi kuolewa na wao wameamua kuishi maisha yao na hawezi kufuatilia maisha ya mtu wala wao kufuatilia maisha ya watu.3

King Lawrenc Arudi Tena na Kudai Mtoto wa Diamond si Wake Bali ni wa Ivan Aliyekuwa Mume wa Zari....

Wakati jina la Latifah mtoto wa Diamond na Zari likizidi kukuwa, rafiki wa karibu wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga, Kinglawrence amemtupia dongo Diamond akisema hakuhitajiki kipimo chochote cha vinasaba DNA ili kujua kuwa, Latifah si mtoto wa Diamond kwani mambo yamejionesha yenyewe baada ya miezi tisa.
Kwenye mtandao wa Instagram, jamaa huyo aliweka picha ya Ivan aliyoiunganisha na picha ya Latifah ili wadau waone walivyofanana. Hapa ana maana kuwa, mtoto huyo ni wa Ivan.

Diamond alipotafutwa aseme neno kuhusiana na madai hayo yote, alipuuza kuhusu mtoto ni wake au si wake, akasema ana furaha iliyopitiliza ya kupata mtoto na kuhusu jina haoni kama kuna tatizo. 3

Diamond Ajivunia Deal la Milioni 50 Alilopewa Bintiye Tiffah, ni Pamoja na Kuvalishwa Bure na Duka Kubwa la Nguo za Watoto

Mtoto wa Diamond Platnumz, Latiffah amepewa endorsement ya shilingi milioni 50 na duka la nguo za watoto ambalo kumvalisha nguo bure ni sehemu ya mkataba huo.


Akiongea jana kwenye hafla iliyoandaliwa na wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete, Diamond alidai kuwa hayo ni sehemu ya maendeleo kwenye muziki yaliyotokea katika mihula miwili ya uongozi wake.

“Katika miaka hii 10 na mtoto nimepata. Mheshimiwa mtoto amezaliwa leo (jana) lakini amepata endorsement leo leo karibuni milioni 50 katika duka tu la kuwa anadhaminiwa kama mtoto anavalishwa na hilo duka, sio maendeleo hayo jamani,?” alihoji Platnumz.

Diamond hakusita pia kuzungumzia rekodi ilivyovunjwa na akaunti ya Instagram ya mwanae, ambayo hadi sasa ina followers zaidi ya elfu 45 siku moja tu baada ya kuzaliwa.

“Katika Afrika ndio mtoto wa kwanza huyo aliyepata followers wengi Afrika nzima, anatokea Tanzania sio maendeleo hayo? 3

Hatimaye Diamond Na Mpenzi Wake Zari Wapata Mtoto Wa Kike.

Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika, Diamond Platnumz amepata  mtoto  wa  kike  toka  kwa  mpenzi  wake  Zari  Hassani.

Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.

Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.


Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.3

Uchawi Wa Naigeria Ndio Siri Ya Mafanikio ya Mwanamuziki Diamond...Lakini Sio Uwezo Wake

Nimekutana na hii Mahali nikaona sio mbaya kushare na ninyi Wadau wangu ..Nanyi mtoe Mtazamo ..

Katika Bara La Afrika.Nigeria Ndo Nje Inayoongoza Kwa Uchawi Na Vitendo Vya Kishirikina.
Wasanii Wakubwa, Wafanybiashara, Wacheza Filamu, Watumishi Wa Mungu, Wanasiasa, Watu Maarufu Nchini Nigeria Achilia Mbali Wananchi Wa Kawaida Wengi Wao Ni Waumini Wa Imani Za Kishetani Na Washirikina Wakubwa.

Mafanikio Ya Ghafla Ya Chibu Na Mlolongo Wa Tuzo.Zinatokana Na Kujihusisha Katika Imani Hizi Za Kinageria.Safari Nyingi Za Chibu Za Kwenda Naigeria Na Kurudi Zinahusisha Pia Kupata Nafasi Ya Kushiriki Katika Ibada Zao Na Kwa Ajili Ya Kutoa Sadaka Na Kufanya Matambiko.

Collabo Nyingi Za Domo Anazoforce Kufanya Na Wanigeria Ni Ktk Muendelezo Wake Wa Kua Karibu Na Wanamuziki Maarufu Ambao Nao Ni Waumini Wa Imani Hizi Za Kichawi.

Inasemekana Hata Utajiri Alionao Mkewe Mtarajiwa Zari(thebosslady) Chimbuko Lake Ni Uko Uko.Siri Ya Pete Ya Dhahabu Anayoivaa Domo Mkono Wake Wa Kushoto Ambayo Wengi Wanadhani Ni Pete Ya Uchumba.Lakini Ukweli Ni Kua Ni Pete Aliyoipata Nchini Nigeria.Na Inabeba Siri Kubwa Ya Mafanikio Yake.

Je kuna Ukweli wowote Juu ya Hii Habari?3

Battle: Kwa Mara Nyingine Tena Wale Mahasimu Wawili wa Bongofleva Nchini Wamekutana TUZO ZA AFRIMMA

Daaah!...ni kwa Mara nyingine tena wale manguli na mahasimu wa BONGOFLEVA nchini...yani ALIKIBA (Ali Saleh Kiba) na DIAMOND PLATNUMZ(Naseeb Abdul Juma) wamekutana kwenye TUZO ZA KIMATAIFA za AFRIMMA AWARDS, Najua teamondi hawaamini na ni ngumu kwao kukubali ila ndo ivyo tena jamaa(KIBA) ndo kashavuka mipaka ya TANZANIA nayeye...hivyo muache kejeli na dharau,Najua mwaka huu AFRIMMA watashangazwa na mvua ya KURA zitakazopigwa ambayo haijawai kutokea kabla na hasa zikitokea TZ na kama kwenye hizi TUZO wao wanapiga pesa basi ni wazi hawatosita kuwarudisha hawa jamaa tena mwakani kwenye kinyanganyiro hicho.

Haya sasa kipenga kimeshalia "TEAMKIBA" na "TEAMMONDI"... Let's go!!!!!

Ingia Hapa Kupiga Kura: http://afrimma.com/nominees-2015/ 3

Nimempata Diamond hapa South Africa, kaeleza ukweli wa beef na Davido na walivyokutana juzi, mtoto wiki ijayo na tuzo za MTV

Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz amekutana na camera ya AyoTV hapa Durban South Africa wakati tukisubiria tuzo za MTV 2015 kaongelea Beef yake na Davido ilivyokua na mpaka wakakutana, mtoto wake wiki ijayo, tuzo za MTV na mengine

3

Nimempata Diamond hapa South Africa, kaeleza ukweli wa beef na Davido na walivyokutana juzi, mtoto wiki ijayo na tuzo za MTV

Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz amekutana na camera ya AyoTV hapa Durban South Africa wakati tukisubiria tuzo za MTV 2015 kaongelea Beef yake na Davido ilivyokua na mpaka wakakutana, mtoto wake wiki ijayo, tuzo za MTV na mengine
3

Video ya Diamond alivyowajibu Waandishi kwenye press ya MTV Awards 2015 hapa Durban South Africa

Kwenye Press conference hapa Durban South Africa Waandishi wa habari wa nchi mbalimbali Afrika na hata wengine wa Uingereza walikua wakihoji mastaa mbalimbali wanaohusika kwenye tuzo hizi akiwemo Diamond Platnumz, Neyo, P Square na wengine ambapo Diamond alijibu maswali kwa kujiamini na kuelezea mambo mbalimbali kwenye hii video hapa chini.

3

Anayedai Kuwa ni Wifi wa Zari Kwa Diamond Azuiwa Getini Kwa Diamond....

Mrembo aliyedai ni dada wa hiyari wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ aliyejitambulisha kwa jina moja la Rose akijiita wifi wa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, hivi karibuni ameumia kupita maelezo baada ya kuzuiwa kuingia nyumbani kwa mastaa hao, Ijumaa lina mkanda mzima.
Rose ambaye ni ‘msichana wa mujini’ alijikuta akitiliwa ngumu na mlinzi nyumbani kwa Diamond maeneo ya Tegeta-Madale, Dar ambapo alikwenda kumuona Zari baada ya kusikia yupo Bongo.

Mlinzi akiwakatalia kuingia ndani.
Kwa mujibu wa Rose, kabla ya Diamond kuwa na uhusiano na Zari walikuwa wapo vizuri lakini baada ya kuwa na mama kijacho huyo, hajawahi kumuona na amekuwa akitamani waonane laivu bila mafanikio.

“Zari ni wifi yangu kwa Diamond (bila kufafanua uwifi kivipi). Pia napenda sana kazi za Diamond lakini tangu waanzishe uhusiano kila ninavyojitahidi niwaone inakuwa ngumu. Ningepata msaada wa kuwaona ningefurahi.
“Nilijaribu kuomba msaada kwa kaka mmoja ambaye ni rafiki wa Diamond lakini akaniambia Zari akiwepo pale nyumbani kwa Diamond hasa kipindi hiki ambacho ni mjamzito, ni ngumu mtu yeyote kuingia,” alisema mrembo huyo.
Ijumaa laamua kumpeleka

Baada ya kushindikana kumuona wifi yake amabaye ni ‘Zari’, Rose aliamua kurudi nyumbani.
Katika kuhakikisha kama alichokuwa akikisema kina ukweli, mmoja wa waandishi wa gazeti hili juzi Jumatano aliamua kumsindikiza Rose hadi nyumbani kwa staa huyo lakini katika hali ya kushangaza, mlinzi binafsi aliyekutwa aliweka ngumu kumfungulia mlango mdada huyo.
“Wewe kama unasema Diamond ni kaka yako na Zari ni wifi yako, ungewapigia simu kabla ya kuja, siwezi kuwafungulia geti,” alisema mlinzi huyo.
Rose: Lakini kaka ungenisaidia tu nikaingia ndani, Diamond akiniona hawezi kunizuia.
Mlinzi: Haiwezekani, tena naomba muondoke.
Kufuatia kuwekewa ngumu huko, mdada huyo aliondoka eneo hilo huku akiwa amenyong’onyea ambapo wakati hayo yote yakiendelea, mmoja wa mapaparazi wetu alikuwa akipiga picha kwa simu ya mkononi.

Kumbe ulinzi mkali
Baada ya dada huyo kutokubaliwa kuingia ndani ya nyumba ya Diamond licha ya kudai ni wifi wa Zari, Ijumaa lilizungumza na baadhi ya watu wanaoishi eneo hilo ambapo walisema ni ngumu sana kupenya kuingia ndani ya mjengo huo.
“Pale bwana wapo wengi wanakuja na kudai ni ndugu wa Diamond lakini wanaishia nje na kuondoka, bila taarifa mlinzi hawezi kukufungulia geti, kwa hiyo kuzuiwa kwa huyo anayedai ni wifi wa Zari siyo ishu,” alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shebe.

DIAMOND ANAMJUA?
Kama kawaida yake ya kutoa ujumbe upande mmoja na kupeleka upande wa pili ili kupata mzani, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alimtafuta Diamond kwa mahewa akiwa kwenye ‘pipa’ kuelekea nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambapo alijibu kwa kifupi: “Nimekwambia simjui huyo dada.”

SIYO ROSE PEKEE
Mbali na Queen Darleen na Esma ambao ni dada zake wa ukweli wanaofahamika, wapo wasichana wengine kibao mjini ambao nao hudai ni dada zake wa hiari ambapo ukimwacha Rose pia yumo Halima Haroun ‘Kimwana’ ambaye hata Zari anamuita wifi licha ya kwamba hana undugu na Diamond.
DIAMOND K
ULAMBA TUZO
Wakati hayo yakiendelea, wikiendi hii Diamond anatarajiwa kulamba tuzo zinazofanyika Sauzi za MTV Music (Mama) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya Msanii Bora wa Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Wimbo Bora wa Kushirikiana Afrika.

KILA LA HERI DIAMOND
Dawati la Ijumaa linamtakia Diamond kila la heri ili ailetee heshima Tanzania katika anga la muziki wa Bongo Fleva. -Mhariri. 3

Natamani mngeelewa jinsi ninavyompenda Zari – Diamond

Diamond Platnumz anatamani watu waelewe jinsi anavyompenda mpenzi wake Zari Tlale aka The Bosslady.

Wawili hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza mwezi ujao.

Hitmaker huyo wa ‘Nana’ amepost picha kwenye Instagram inayomuonesha akilibusu tumbo la mpenzi wake huyo na kuandika, “I wish you can understand how Much i Love this Woman… Thanks God for the life have always prayed for."

Msanii huyo amemaanisha, “Natamani mngeelewa jinsi ninavyompenda huyu mwanamke. Asante Mungu kwa maisha niliyokuwa nikiyaomba siku zote.”

3
Ni utamaduni wa kawaida kwenye nchi zilizoendelea au nchi kubwa duniani Wasanii kulipwa pesa kutokana na nyimbo zao kuchezwa kwenye TV na Radio ambapo hii imemtokea Mtanzania Diamond Platnumz baada ya wimbo wake kuchezwa kwenye TV maarufu kwa burudani, BET ya Marekani.

Tazama hii video hapa chini ujue hizo milioni alizozichukua Diamond.
3

Producer Manecky na Diamond Platnumz Wamaliza Tofauti zao, Waamua Kufanya Kitu Hichi Pamoja

Mtayarishaji wa muziki wa AM records, Manecky na Diamond Platnumz wamemaliza tofauti zao.

Manecky ameiambia Bongo5 kuwa ameanza kurekodi tena na Diamond baada ya miaka takriban miwili ya kutofanya kazi pamoja.

“Unajua kuna mzingira fulani yalijitokeza kati yangu mimi na Diamond tukawa muda mrefu sana hatujaongea na kuonana na kufanya kitu,” mtayarishaji huyo ameiambia Bongo5.

“Unajua kuna time inafika kila mtu anagundua ana mapungufu yake, sasa mnapoamua kuachana na mambo hayo mnaachana nayo. Sasa mimi sioni kama kuna sababu ya kukaa tena chini na kumuangalia nani alikosea. Sasa hivi tunasonga kwenda mbele, sasa hivi tupo fresh ndio maana tumeshaanza kurekodi ngoma mpya na Nay wa Mitego ili kutengeneza kitu kizuri,” ameongeza Manecky.

Hata hivyo Manecky amesema bado anapata wakati mgumu kuitafuta chemistry yake na Diamond kwakuwa ni kipindi kirefu hawajafanya kazi pamoja.

“Sasa hivi napata wakati fulani mgumu, unajua tumekaa muda mrefu hatujaonana wala kuongea/ Utajikuta unafanya kazi kwa mazingira fulani ili upate kitu kizuri ili kazi iwe nzuri.” 3

Nyota ya Diamond Platnumz Inazidi Kung'ara.......Katajwa Kuwania Tuzo za Uganda (Uganda Entertainment Awards 2015 )

Diamond Platnumz ameendelea kutajwa kuwania tuzo mbalimbali barani Afrika.

Akiwa ni miongoni mwa wanaowania tuzo za MAMA zitakazotolewa mwezi huu, muimbaji huyo wa ‘Nana’ ametajwa kuwania tuzo zingine za Uganda zijulikanazo kama Uganda Entertainment Awards 2015 (UEA)

Platnumz anawania kipengele cha Best African Act akichuana na Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria) na Active

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort (Speke Ball) jijini Kampala, Uganda. 3

Diamond Platnumz Akiri Kumpenda Omotola wa Nigeria

Omotola
KING wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametengeneza kichwa cha habari nchini Nigeria baada ya kufunguka kuwa anampenda ‘vibaya’ staa wa filamu nchini humo, Omotola Jalade Ekeinde

Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond katika ziara ya kimuziki iitwayo ‘Nana Tour’ nchini humo, staa huyo ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mjasiamali maarufu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amekuwa akiumizwa na penzi la Omotola kitambo sana lakini hakuwahi kuzungumza katika vyombo vya habari.

Diamond Platnumz

  • “Diamond ana maumbo yake flani hivi amazing ambayo huwa anayapenda, siku nyingi sana kabla hata hajakutana na Zari, alikuwa akituambia watu wake wa karibu kwamba miongoni mwa wanawake mastaa ambao anawatamani awaweke kwenye himaya ya penzi lake ni Omotola.



  • “Alisema anampenda kwa kila kitu kuanzia ufanyaji kazi wake, umbo lake na hata umaarufu mkubwa alionao ndani na nje ya Bara la Afrika,” kilisema chanzo hicho.


Baada ya chanzo hicho kueleza habari hiyo, mapema wiki hii, mtandao wa nigeriafilms.com ulithibitisha maneno hayo kwa kuposti habari iliyobainisha Diamond anampenda Omotola sanjari na mastaa wengine wawili wa Nigeria anaovutiwa nao kimapenzi.

Akiwa hewani alipokuwa akihojiwa na redio moja jijini Lagos, Diamond aliweka bayana kuwa anateswa na penzi la mastaa watatu Nigeria, Omotola, Tonto Dikeh na Genevieve Nnaji.


  • “Jamaa kitambo sana anateswa na penzi la Omotola sasa leo kaongeza na wengine wawili na ninavyomjua hashindwi kufanya kweli ingawa nina wasiwasi kwa Omotola na Tonto maana wana waume zao labda ajiweke kwa Genevieve ambaye hajaolewa,” kilikazia chanzo chetu.


Diamond hakupatikana ili kusikia kauli yake juu ya ishu hiyo.

Chanzo: GPL 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips