Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Producer Manecky na Diamond Platnumz Wamaliza Tofauti zao, Waamua Kufanya Kitu Hichi Pamoja

Producer Manecky na Diamond Platnumz Wamaliza Tofauti zao, Waamua Kufanya Kitu Hichi Pamoja

Mtayarishaji wa muziki wa AM records, Manecky na Diamond Platnumz wamemaliza tofauti zao.

Manecky ameiambia Bongo5 kuwa ameanza kurekodi tena na Diamond baada ya miaka takriban miwili ya kutofanya kazi pamoja.

“Unajua kuna mzingira fulani yalijitokeza kati yangu mimi na Diamond tukawa muda mrefu sana hatujaongea na kuonana na kufanya kitu,” mtayarishaji huyo ameiambia Bongo5.

“Unajua kuna time inafika kila mtu anagundua ana mapungufu yake, sasa mnapoamua kuachana na mambo hayo mnaachana nayo. Sasa mimi sioni kama kuna sababu ya kukaa tena chini na kumuangalia nani alikosea. Sasa hivi tunasonga kwenda mbele, sasa hivi tupo fresh ndio maana tumeshaanza kurekodi ngoma mpya na Nay wa Mitego ili kutengeneza kitu kizuri,” ameongeza Manecky.

Hata hivyo Manecky amesema bado anapata wakati mgumu kuitafuta chemistry yake na Diamond kwakuwa ni kipindi kirefu hawajafanya kazi pamoja.

“Sasa hivi napata wakati fulani mgumu, unajua tumekaa muda mrefu hatujaonana wala kuongea/ Utajikuta unafanya kazi kwa mazingira fulani ili upate kitu kizuri ili kazi iwe nzuri.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips