Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Zari The Lady Boss. Show all posts
Showing posts with label Zari The Lady Boss. Show all posts

Picha za Shoo ya Diamond Platnumz Alivyowasha Moto Kwenye Concert Nchini Uganda..Zari Naye Alikuwepo

Usiku wa jana msanii Diamond Platinum alitumbuiza kwenye tamsasha kubwa ‘Born 2 Win Concert’ jijIni Kampala, Uganda.
Mbali na Diamond msanii Patoranking naye alitumbuiza kwenye tamasha hilo.

Hizi ni baadhi ya picha za Diamond akitumbuiza kwenye tamasha hilo.
DIAMOND13
Diamond1341DIAMOND134DIAMOND288DIAMOND186
3

Diamond Platnumz Aikacha Party ya Zari All White Ciroc Party, Ex wa Zari na Wapambe Wake Wahuzuria, Picha Hizi Hapa

Wana watoto watatu pamoja na wana biashara kibao za pamoja, hivyo ni ngumu kwa Zari na mume wake wake wa zamani, Ivan kupotezeana licha ya kila mmoja kuchukua njia yake kimahusiano.

Ivan na jamaa zake wa Rich Gang wakila bata kwenye Zari All White Party

Ndio maana Ivan na mpambe wake King Lawrenc walisafiri kutoka SA na kwenda kumuunga mkono Zari ambaye Alhamis hii aliandaa party yake ya kila mwaka ya mavazi meupe tu kwenye kiota cha Guvnor kilichopo Kampala Uganda.

Zari All White Ciroc Party
Zari All White Ciroc Party

ZARI8912ZARI834ZARI234ZARI734


ZARI0923


ZARI13

ZARI90

TOA 3

Zari is in South Africa…..She Shares These Photos With Her All 4 children

Raphael_rich21...so calm and collected. He ma main soldier



And finally with ma Manchester soccer academy player @pinto_bitw. The most shy person ive ever known, very humble and very smart. Mummy is very short soon y'all be looking in ma head...... where ma high heels at???
3

Photos: Mama Zari Visits Diamond And Zari In Dar To See Granddaughter Tiffah Dangote.

Zari
Mama Zari flew from Uganda to Tanzania this weekend to see her granddaughter Tiffah Platnumz Dangote who was born 3 weeks ago, And do you see the stunning home of Diamond and Zari ...!


3

Madai Mtoto si wa Diamond, Zari Aitwa Kwao Uganda

KIMENUKA! Baada ya madai kwamba mtoto Latifah ‘Tiffah’ si damu ya Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku shemeji wa zamani wa Zarinah Hassan ‘Zari’ (mama Tiffah), King Lawrence naye kusema mtoto huyo ni wake, kuna taarifa mpya zinazodai kuwa, Zari ameitwa kwao, Uganda ili akamalize ubishi juu ya suala hilo, Risasi Jumamosi limenasa mchapo kamili.
Hivi karibuni baada ya Zari kujifungua, King Lawrence alijitokeza na kudai kuwa, mtoto huyo ni wake na kusema kama kuna anayebisha kiitishwe kipimo cha vinasaba (DNA), hivyo kuibua mkanganyiko na taarifa zilizozagaa awali kuwa, mtoto huyo ni wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, hivi karibuni, Zari alipigiwa simu na mama yake mzazi, Halima Hassan akimtaka aende nyumbani kwao ili akawaeleze ukweli ndugu zake ambao wamekuwa njia panda baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba Tiffah si wa Diamond ambaye familia inamtambua kwa sasa.
“Taarifa zinawafikia tofauti. Kuna zile za awali kwamba mtoto huyo ni wa Ivan, mara zikaibuka nyingine kwamba ni wa King Lawrence hivyo mama amemuita Zari ili akategue kitendawili hicho kumaliza ubishi.

ATAKIWA KWENDA NA UKWELI
“Amemtaka aende na ukweli moyoni maana yeye (Zari) ndiye anayeujua. Hata hiyo DNA haina maana. Ameambiwa kwamba siku zote mama ndiye anayejua ukweli wa mtoto ni wa nani,” kilisema chanzo hicho.

ATAKIWA AMUOGOPE MUNGU
Chanzo kilizidi kunyetisha kuwa, mbali na kumtaka aende na ukweli, familia imemtahadharisha atakapofika aseme ukweli kwa kumuogopa Mungu maana vinginevyo dhambi hiyo itamhukumu maisha yake yote.
“Ametahadharishwa na familia kwamba anapaswa kumuogopa Mungu maana ni dhambi mtoto wa baba huyu kumpa baba huyu. Wao Kama familia wanajua Tiffah ni wa Diamond. Sasa wanakangaywa na hao wanaodai wao ndiyo haswa wahusika.

HAWAHOFII KAMA SI WA DIAMOND
“Familia imesema haina shida hata kama itakuwa mtoto si wa Diamond lakini wanachotaka wao ni kujua ukweli tu.” Chanzo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya King Lawrence kuibuka na barua ya wakili kuitisha kipimo cha DNA akidai mtoto ni wake, Diamond alisisitiza kwamba mtoto huyo ni damu yake hivyo hana muda wa kubishana na mtu.

“Huyo jamaa (King Lawrence) atakuwa anatafuta kiki katika vyombo vya habari. Huyohuyo ndiye alianza kusema mtoto si wangu ni wa Ivan mara amegeuka tena na kusema ni wake yeye, hata haeleweki. Siwezi kujibishana naye.
“Hata hiyo barua aliyosema ni ya wakili ya kutaka DNA, haijatufikia! Nasikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alisema Diamond.

KUHUSU SAFARI
Alipotafutwa Diamond ili aeleze kuhusu taarifa za mama Tiffah kuitwa nchini Uganda ili akaeleze ukweli, alisema hayo ni mambo ya kifamilia zaidi na hata hivyo haoni tatizo ndugu kumwita Zari kwani ukweli Tiffah ni damu yake na hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea.
“Tiffah ni damu yangu hata akienda hakuna kitakachobadilika. Sina wasiwasi maana mimi najua mahesabu yake yote na ninajua mpaka tarehe niliyokutana naye na mtoto akawepo,” alisema Diamond huku akisema, Zari hana nafasi ya kuongea na vyombo vya habari.

NCHINI UGANDA
Nchini Uganda, bado baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti mkanganyiko wa mtoto wa Diamond ambapo baadhi ya magazeti yametaka Zari aende akapime DNA ili kujiridhisha kuhusu uhalisia.

AFRIKA KUSINI
Nazo habari kutoka nchini Afrika Kusini ambako ndiko kwenye makazi ya Zari, baadhi ya Wabongo wanaoishi jirani na Zari walisema wanatambua uwepo wa Diamond kama mpenzi mpya wa Zari kwa hiyo hakuna shaka kuwa yeye ndiye baba (biological father) wa Tiffah.
Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu juzi, mkazi mmoja wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Steve, alisema amekuwa akimfuatilia kwa karibu King Lawrence kupitia Instagram yake akidai kwamba yeye ni baba wa Tiffah, lakini sehemu kubwa ya watu wenye ujirani na Zari kule wanaamini, Diamond ndiye baba husika.

“Kuhusu Diamond kuwa baba wa Latifah hilo halina ubishi. Hata sisi huku tunajua hivyo. Hili suala liangaliwe kwa macho matatu. Nahisi kuna ‘vita’ ya sisi Watanzania na Waganda kuhusu mtoto,” alisema Mbongo huyo.

Source:Globalpublishers 3

Hatimaye Diamond Na Mpenzi Wake Zari Wapata Mtoto Wa Kike.

Staa wa Bongo Fleva ambaye jina lake limebeba uzito mkubwa Afrika, Diamond Platnumz amepata  mtoto  wa  kike  toka  kwa  mpenzi  wake  Zari  Hassani.

Mtoto huyo ameingia duniani saa 10 na dakika 40 Alfajir, Alhamis hii.

Haijaweza kufahamika kwa mara moja ni hospitali gani mtoto huyo amezaliwa kwa kile meneja alichosema ‘usalama wa mama na mtoto’ kwakuwa bado wapo hospitali.

Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu, karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” ameandika Diamond kwenye picha hiyo juu aliyoiweka Instagram.


Awali Diamond alisema kuwa Zari angejifungulia Tanzania.3

Mume Wa Zari Abambikiwa Mimba na Msichana Mtangazaji wa TV....Alitaka Kulipa Kisasi kwa Zari ....

Wakati staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akisubiri mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ajifungue mtoto wa kike ‘taimu’ yoyote kutoka sasa, aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kubambikiwa mimba na mtangazaji wa runinga aitwaye Doreen Kumhangi, Ijumaa limeidaka.

TUJIUNGE JIJINI KAMPALA
Habari kutoka jijini Kampala, Mji Mkuu wa Uganda zilidai kwamba, Ivan na Doreen ambaye ni Mtangazaji wa Kipindi cha Morning Breeze cha Televisheni ya NBS ya Uganda, wamekuwa wakionekana wakiwa wamegandana kama ruba kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka jana.
dd“Muda wote Ivan akiwa Kampala anajirusha na Doreen. Mara kadhaa wameonekana viwanja tofauti wakila bata. Hata Doreen anapokwenda South Africa (Sauz) amekuwa akipokelewa na Ivan ambaye ana makazi mengine huko kisha kufanya yao,” kilidai chanzo ambacho ni mfuatiliaji wa masuala ya burudani nchini Uganda.

DOREEN ATOA SIRI NZITO
Ilidaiwa kwamba, baada ya bata zote hizo, hivi karibuni, Doreen alitoa siri nzito kuwa ana ujauzito uliosababishwa na Ivan, jambo lililomfanya jamaa huyo ‘kupaniki’.
Ilisemekana kwamba, kufuatia Ivan kukanusha kwa nguvu zote, kuna madai kwamba Doreen anambambikia mimba hiyo akiamini kwamba watu watakubaliana naye kwa kuwa ndiye amekuwa naye katika kipindi alichonasa mimba.

ALITAKA KULIPA KISASI KWA ZARI?
Katika mapenzi yao, ilielezwa kuwa, kuna kipindi Ivan alitaka kumhalalisha Doreen kuwa mkewe na haikujulikana ishu hiyo iliishia wapi huku nyuma kukiwa na madai kwamba alitaka kumrusha roho au kumlipiza Zari.
“Sijawahi kutembea na Doreen kwa hiyo mimi sihusiki na ujauzito alionao,” alisema Ivan juzikati alipobanwa na gazeti moja nchini humo.
“Anachokisema (Doreen) si kweli, anataka kunibambikia mimba,” alisema jamaa huyo aliyezaa na Zari watoto watatu wa kiume huku akiendelea kukanusha ishu hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Instagram.

DOREEN NI NANI?
Habari zilieleza kwamba, Doreen ni mtangazaji anayesoma habari kwenye kipindi hicho cha asubuhi cha NBSTV.
Kabla ya kudaiwa kuwa na Ivan, Doreen alikuwa shosti wa karibu na Zari na kwamba walishafanya kazi pamoja ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema ndiye mbadala sahihi wa Zari kwa jamaa huyo.

FAMILIA YA DIAMOND CHEREKO
Wakati hayo yakiendelea kwa Ivan, jijini Dar chereko zinasubiriwa za kumpokea mgeni kwenye familia ya Diamond ikielezwa kwamba Zari atajifungua muda wowote kutoka sasa. 3

This is What Zari Post On Her Instagram Account....

This is What Zari Post On Her Instagram Account....3

Natamani mngeelewa jinsi ninavyompenda Zari – Diamond

Diamond Platnumz anatamani watu waelewe jinsi anavyompenda mpenzi wake Zari Tlale aka The Bosslady.

Wawili hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza mwezi ujao.

Hitmaker huyo wa ‘Nana’ amepost picha kwenye Instagram inayomuonesha akilibusu tumbo la mpenzi wake huyo na kuandika, “I wish you can understand how Much i Love this Woman… Thanks God for the life have always prayed for."

Msanii huyo amemaanisha, “Natamani mngeelewa jinsi ninavyompenda huyu mwanamke. Asante Mungu kwa maisha niliyokuwa nikiyaomba siku zote.”

3

Msichana Anayemzimikia Diamond Platnumz Kimapenzi Awaomba Watanzania Wamuuonge Mkono..Adai yeye ni Natural Kuliko Zari

Watanzania munisuport Mimi Tanzania mwenzenu...... uyo Mgandaa ni 360 watanzania wotee ni nduguu mali za watanzinia zitumiwee na wataniaa iwejee MTU from no where atuchukulie kijana wetuu mnajua Tanzania hairuhuruu urai wa nchi mbili what if diamond akiamua kufunga ndoa na zari Diamond akachukua Uraia wa South ili wamlee mtoto hamuoni atakua tumepoteza icon... muni support nimpate dai tuoanee atabakia kwetu..... nipigieni kura Mumtagg Diamond najua akiniona niko natural atanitongoza....By Baby_ake

Pia amepost picha hii na kuandika haya:
Mrs and mr D..... Msinitukanee eti mnasema nimechanganyikiwa.. yes nimechanganyikiwa kimapenzi you cant tell me nothing.. yaani MTU akinivunja moyo now ntamtukama matusii yanguoni sijawahi mtukana MTU but mnanilazimisha
Basi mwenzenuu Leo nimeota niko Kitanda kimoja na Diamond ..... haha nimeonja muogo wake wa jangombe  ni mtamu . .... yaani tume last 45 kiu yoote kaikata. . .. kushtuka ni ndoto but i hope. Itakua kweli. I LOVE you D
Team baby ake mpooooooooooooo?
3

DIAMOND is lucky to have ZARI as his baby mama…. look at how she treats her sons

"God thank You for all our blessings and favor today..... movie.... night in Raphaels' room. Nyt africa"
3

This is new Car of Diamond Platnumz Given By his Baby Zari

Gift from Zari to Diamond Platnumz...
Diamondplatnumz Captioned The Above Pic as Follows:
Thanks alot baby it's Finaly Here ���� @zarithebosslady
3

Zari za Boss Lady Anaishi Nyumba Moja na Ivan Aliyekuwa Mmewe Huko South Africa..Ushahidi Huu Hapa

Zarina Hassan A.K.A Zari the boss lady mama kijacho wa Diamond Platnum hajawahi kumpeleka mpenzi wake huyo nchini South Africa anakoishi.Sababu Zari anaishi nyumba moja na mme wake Ivan aliyezaa nae watoto wa tatu.Ushahidi wa kuishi pamoja ni hizi picha ambazo hata mahakamani ushahidi wa picha unakubalika.Swimming pool tiles zake za pembeni hapo juu ni zilele zile za hapo chini alipokaa mme huyo wa Zari.Pili rangi ya ukuta alio chuchumaa Zari hapo juu ni ya creem sawa sawa na ukuta wa chini aliokaa mme mwenza wa Diamond Platnum.Tatu picha ya chini Zari akiwa parking rangi za ukuta ni sawa na nyumba aliyokaa kibopa huyo.
3

This is Why Zari will be a s3xy Mama Forever....Gym grind....Photos

Sometimes God's silence is the most loving and beautiful gift He gives to us, becoz it causes us to grow, stretch, trust & believe....Yeeeeeaaassss she still about that life Gym Grind- Zari

3

Zari Ajitetea 'Mimi Sio Msagaji ilitokea tu Nikakisi na Msichana Mwenzangu kwa katika Hali ya Furaha'

Super star kiwango anayetikisa East Africa kwa sasa , zarinah hassan aka bossy lady, amefunguka kuhusu scandal ya usagaji iliyomtafuna miezi michache iliyopita, akizungumza kupitia kipindi cha sporah show, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake alifunguka kuhusu kashfa hyo, ambapo picha yake akiwa kwenye mahaba na mrembo mwenzie zilisambazwa mitandaoni na kuzua gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii

Mwenyewe alijitetea kuwa walikuwa kwenye starehe zao yeye pamoja rafiki zake, ambapo kila mtu alikuwa na mpenzi wake, so ilitokea tu wakajikuta wamekisi na rafiki yake huyo wa kike katika hali ya furaha kama marafiki wengine tu, na hakufikiria kuwa lile tukio lingekuwa ishu sana kwenye mitandao. aliendelea kutiririka kuwa yeye sio msagaji na anapenda wanaume kama wasichana wengine 3

Diamond: Tumeshapima DNA na kujua mtoto ni wa kike

Bwana mdogo Huyu alipokuwa anahojiwa na mtangazaji wa BBC na kuulizwa swali kama ameshajua Jinsia ha mtoto kwa kushangaza kabisa alijibu yes tumeshapima DNA na kujua mtoto wa ni wa kike.ushauri wangu kwa Dogo kwa kusema ukweli ame emprove sana kwenye Lugha Ila tatizo ni mbwembwe na uongo akiacha Uongo na mbwembwe lazima tutegemee makubwa zaidi toka kwake.3

Zari wa Diamond Ateswa na Picha Inayoonyesha Akiwa Beneti na Pedeshee Katunzi

MUSA MATEJA
MCHUMBA wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,  Zarina Hassan ‘Zari’ amedaiwa kuangua kilio baada ya kuvuja kwa picha yake na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Mzamili Katunzi ambayo ilidaiwa kuwa ni mtu wake na kusababisha gumzo mjini.

Mtu wa karibu na Zari amefunguka kuwa Zari alijisikia vibaya sana baada ya kuona picha hiyo na kukasirika hivyo kuanza kuwasaka watu walioivujisha kwani walikuwa na nia mbaya ya kumgombanisha lakini wamechemka.
Zari kamaindi kweli, anajiuliza huyo aliyeivujisha alikuwa na lengo gani?” alisema mtu huyo

Jitihada za kuzungumza na Zari hazikuzaa matunda lakini bahati nzuri Diamond alipatikana na kufafanua:
 “Ni kweli zimemsumbua baby lakini nimemuweka sawa kwa kuwa najua ni mambo ya mitandao, hakuna ukweli wowote.” 3

Mume wa Zari Ivan Anaswa Kwa Shosti wa Zari Ambaye ni Model Maarufu Uganda

Kampala, Uganda
Habari kutoka nyumba ya jirani nchini Uganda ikufikie kwamba aliyekuwa mume wa mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, tajiri Ivan Ssemwanga anadaiwa kunasa penzi la shosti wa kufa na kuzikana wa mkewe huyo aitwaye Stella Nankya, Ijumaa Wikienda limetonywa.


Ubuyu kutoka jijini Kampala nchini humo ulidadavua kwamba, Ivan na Stella ambaye ni modo maarufu wa Uganda na Afrika Kusini ‘Sauzi’, hivi karibuni wamekuwa wakijiachia kimalovee kwa raha zao.

Tukio la juzikati lililoacha gumzo ni pale wawili hao waliponaswa wakiwa wamegandana kimahaba kwenye Ukumbi wa Ekitone uliopo Pretoria nchini Afrika Kusini ambapo kulikuwa na tamasha la muziki.

“Walikaa pamoja, walijiachia pamoja ziro ‘distansi’ kwani hakukuwa na kitu cha kuwatenganisha kati yao. Kwa kweli walionekana ‘kapo’ ya kupendeza mno,” alisema shuhuda wa tukio hilo na kukaririwa na gazeti moja la nchini Uganda.

Kufuatia urafiki wa Stella na Zari walivyokuwa wameshibana, mashabiki wao wamekuwa na maoni tofauti huku Stella akionekana msaliti kwa Zari.

Habari nyingine zilidai kwamba, Ivan ameamua kufanya hivyo ikiwa kama kisasi au kumrusha roho Zari aliyezaa naye watoto watatu ambapo anatarajia kumzalia Diamond siku chache zijazo.

Ilielezwa kuwa, Stella alipoulizwa kwa nini ameamua kumsaliti rafiki yake Zari kwa kutembea na Ivan alisema kwa kifupi:

“Sitaki kuwa karibu na mtu mkavu (Zari), na mimi nimeamua kuwa mkavu.”

Zari au mama kijacho na Stella walikuwa ni marafiki wakubwa ambapo kuna wakati Zari alimpa sapoti ya nguvu Stella alipokwenda kuiwakilisha Uganda kwenye mashindano ya urembo ya Miss Asia Pacific huko Seoul nchini Korea Kusini ambapo walisafiri wote. 3

Barua Nzito Wema Kuna Kitu cha Kujifunza kwa‭ ‬Zari‭!

KWAKO mtoto mzuri, Beutiful Onyinye, Wema Sepetu !'Madam'. Vipi uko poa? Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima namshukuru Mungu, hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa maisha yangu.

Kitambo kidogo hatujaonana, nimeona si mbaya kama nitakukumbuka kwa barua maana najua kutokana na majukumu yako na yangu kuwa mengi, wakati mwingine tunaweza tukafikisha hata miezi sita hatujaonana.

Dhumuni la barua hii ni kutaka kukushauri kwamba unaweza kujifunza kitu kutoka kwa mpenzi wa sasa wa aliyekuwa mpenzi wako, Nasibu Abdul !'Diamond, Zarinah Hassan !'Zari!

Naomba usinielewe vibaya. Sina nia ya kukupambanisha wala kutaka kukukejeli kwa namna yoyote. Kuna kitu kidogo tu cha kujifunza kutoka kwa binti huyo wa Kiganda.
Achana na maneno yanayosemwa mtaani, kila mmoja ana upungufu wake lakini binadamu tunashauriwa kuiga yale mazuri kutoka kwa wenzetu.

Iko hivi Wema, wewe na yeye mna nafasi moja nzuri katika jamii. Nyinyi ni maarufu. Mnapendwa na watu kupita maelezo. Mna ushawishi mkubwa sana katika jamii hivyo mnaweza kufanya jambo na likapata mafanikio makubwa sana.

Umaarufu wenu ni biashara. Kwa nini uendelee kubaki chini wakati umezungukwa na fursa kibao? Umaarufu wako ni biashara kama utaamua kuwa !٪serious!& na kila hatua unayoipiga.
Nikwambie ukweli bila unafiki, unapaswa kuiga jambo moja tu la msingi kutoka kwa Zari, kuwekeza na kuheshimu fedha.

Mwenzako anaijua fedha. Anajua namna ya kuitafuta na namna ya kuiwekeza katika maeneo ambayo yatazidi kuzizalisha. Akili yake inawaza pesa na si starehe zisizokuwa na msingi.
Mfano mdogo tu ni !٪idea!& kama ya All White Party aliyofanya Zari kule Uganda. Alifanikiwa, anaendelea kufanya na wiki iliyopita aliifanya pale Mlimani City jijini Dar na kupata mafanikio makubwa.

Kwangu mimi kile ni kitu kikubwa sana ambacho kinaingiza fedha nyingi kwa wakati mmoja. Si vibaya kama utaiga vitu vya namna hiyo. Nisikufiche, nafasi ya umaarufu uliyonayo Kibongobongo, unaweza kufanya zaidi ya shoo ile kama utaamua na kupata watu wazuri wa kufanya nao kazi.

Na unapofanya mambo makubwa kama hayo, lazima pia udhibiti matumizi yako. Starehe zipo lakini wakati mwingine unapaswa kuheshimu fedha. Yale mambo ya kwenda kuzimwaga ukumbini eti kuwa kama kina pedeshee !٪nanilii!&, si mazuri.

Jeuri ya fedha ifanye kwa kufungua miradi mikubwa ambayo hata utakapozeeka utainjoi matunda yake. Kuigiza kuna mwisho, huwezi kuwa mwigizaji milele, kuna wakati utatakiwa kuwa msimamizi wa miradi yako tu binafsi na mkono uende kinywani kiulani tu.

Usikubali kushikiwa akili na wapambe, unayoshauriwa na wapambe yachuje maana si yote yanakuwa na manufaa. Tumia kipaji na jina lako vizuri, una nyota ya kupendwa basi kupendwa huko kuwe na faida.
Natambua una idea zako ambazo tayari umeanzisha kama kipindi chako cha In My Shoes, usiishie hapo fanya makubwa zaidi.
Kwa leo acha niishie hapo. Ni matumaini umenielewa.
Wasalaam3

Eti Wema Mrembo Kuliko Zari!

Imebainika kuwa maneno ‘gold digger’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri) kwenye maisha.

Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi.

Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake, Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.

Gazeti la Ijumaa liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza kwenye show yakewakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.

Kwa mujibu wa mashabiki hao, picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa) na kwamba ukimuona ‘live’ huwezi kuamini.

“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.

“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa. Wema ni habari nyingine,” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.

“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa,” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari.

“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make-up (vipodozi) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema) hata asipotumia make-up lazima utampenda tu,” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.

Kuhusu make-up, gazeti hilo lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make-up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.

Mdau mwingine aliliambia gazeti hilo kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.

“Ameona fursa kwa Diamond. Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘koneksheni’ na Diamond,” alidai mdau mwingine.

Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.

Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka:

“Tutaishi hapahapa (Bongo). Kwa utamaduni wetu (Waafrika) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote.

“Watanzania ni watu poa sana, siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana.”

Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.

Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.

Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda, mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala, Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Moze Radio na  Weasel, Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, DJ Shiru, mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

GPL 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips