Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » Eti Wema Mrembo Kuliko Zari!

Eti Wema Mrembo Kuliko Zari!

Imebainika kuwa maneno ‘gold digger’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri) kwenye maisha.

Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi.

Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake, Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.

Gazeti la Ijumaa liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza kwenye show yakewakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.

Kwa mujibu wa mashabiki hao, picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa) na kwamba ukimuona ‘live’ huwezi kuamini.

“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.

“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa. Wema ni habari nyingine,” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.

“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa,” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari.

“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make-up (vipodozi) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema) hata asipotumia make-up lazima utampenda tu,” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.

Kuhusu make-up, gazeti hilo lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make-up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.

Mdau mwingine aliliambia gazeti hilo kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.

“Ameona fursa kwa Diamond. Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘koneksheni’ na Diamond,” alidai mdau mwingine.

Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.

Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka:

“Tutaishi hapahapa (Bongo). Kwa utamaduni wetu (Waafrika) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote.

“Watanzania ni watu poa sana, siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana.”

Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.

Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.

Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda, mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala, Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Moze Radio na  Weasel, Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, DJ Shiru, mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

GPL WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips