Ushindi wa bao 1-0 kwa Chelsea dhidi ya Crystal Palace umeitangazia ubingwa klabu hiyo na sasa ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya England.
Kwa ushindi huo, Chelsea imefikisha pointi 83 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi hiyo.
Kabla ya mchezo wao wa jana mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Dider Drogba
alionyesha hisia zake za kutaka kufunga katika mchezo huo ili
kuhitimisha ubingwa wao lakini bahati haikuwa yake na badala yake bao
pekee la ushindi lilifungwa na Eden Hazard.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge maarufu kama darajani, Chelsea walipata bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao Eden Hazard ambaye alipiga mkwaju wa penalti ukaokolewa na kipa lakini mpira ukamkuta tena yeye na kumalizia kwa kichwa.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment