TUJIUNGE JIJINI KAMPALA
Habari kutoka jijini Kampala, Mji Mkuu wa Uganda zilidai kwamba, Ivan na Doreen ambaye ni Mtangazaji wa Kipindi cha Morning Breeze cha Televisheni ya NBS ya Uganda, wamekuwa wakionekana wakiwa wamegandana kama ruba kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka jana.
dd“Muda wote Ivan akiwa Kampala anajirusha na Doreen. Mara kadhaa wameonekana viwanja tofauti wakila bata. Hata Doreen anapokwenda South Africa (Sauz) amekuwa akipokelewa na Ivan ambaye ana makazi mengine huko kisha kufanya yao,” kilidai chanzo ambacho ni mfuatiliaji wa masuala ya burudani nchini Uganda.
DOREEN ATOA SIRI NZITO
Ilidaiwa kwamba, baada ya bata zote hizo, hivi karibuni, Doreen alitoa siri nzito kuwa ana ujauzito uliosababishwa na Ivan, jambo lililomfanya jamaa huyo ‘kupaniki’.
Ilisemekana kwamba, kufuatia Ivan kukanusha kwa nguvu zote, kuna madai kwamba Doreen anambambikia mimba hiyo akiamini kwamba watu watakubaliana naye kwa kuwa ndiye amekuwa naye katika kipindi alichonasa mimba.
ALITAKA KULIPA KISASI KWA ZARI?
Katika mapenzi yao, ilielezwa kuwa, kuna kipindi Ivan alitaka kumhalalisha Doreen kuwa mkewe na haikujulikana ishu hiyo iliishia wapi huku nyuma kukiwa na madai kwamba alitaka kumrusha roho au kumlipiza Zari.
“Sijawahi kutembea na Doreen kwa hiyo mimi sihusiki na ujauzito alionao,” alisema Ivan juzikati alipobanwa na gazeti moja nchini humo.
“Anachokisema (Doreen) si kweli, anataka kunibambikia mimba,” alisema jamaa huyo aliyezaa na Zari watoto watatu wa kiume huku akiendelea kukanusha ishu hiyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Instagram.
DOREEN NI NANI?
Habari zilieleza kwamba, Doreen ni mtangazaji anayesoma habari kwenye kipindi hicho cha asubuhi cha NBSTV.
Kabla ya kudaiwa kuwa na Ivan, Doreen alikuwa shosti wa karibu na Zari na kwamba walishafanya kazi pamoja ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema ndiye mbadala sahihi wa Zari kwa jamaa huyo.
FAMILIA YA DIAMOND CHEREKO
Wakati hayo yakiendelea kwa Ivan, jijini Dar chereko zinasubiriwa za kumpokea mgeni kwenye familia ya Diamond ikielezwa kwamba Zari atajifungua muda wowote kutoka sasa. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment