Yapo makundi ambayo ni mazuri ila huwezi kujiingiza kichwa kichwa eti umeumizwa na boyfriend unalia lia kwenye whatsap groups kwani huyo mumeo? Yaan unajifunuaaa maisha yako yote kwa watu ambao si mamako au ndugu yako. Jaman!!! Wengine mnafundishwa jinsi ya kufanya mapenzi na kuweka madude kibao sehemu za siri...seriously? ?? Hapo hujaolewa..baadae ukikutwa na kansa ya kizazi? Jitihada zoote halafu asikuoe?? Utasingizia kungwi wa whatsapp ukute hata hujawahi kuonana naye?
Kama unataka kufundwa muulize mzazi wako au mtu mzima au jichagulie mtu mmoja utakayemwamini sana hakuna siri zaidi ya watu wawili, soma vitabu mbali mbali khs mahusiano au hapana soma vitabu vya dini vimeeleza kila hatua ya kuishi na mwenzi wako. Mnatozwa pesa huko whatsap halafu mambo bado hayaendi unavyotaka unabaki kulalamika...tatizo ni UFAHAMU wako. Samahan simharibii mtu biashara yake ila acheni kutumia madhaifu ya wengine kama dampo la kuwapoteza zaidi, kwanini usiwasiliane na mtu binafsi mpaka kumuunganisha kwenye magroup?
Jifunzeni kutunza siri zenu. Usimuamini kila mtu.
Mrekebisha TabiaWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment