Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Taarifa ya Jeshi la Polisi Nchini Kufuatia Upotoshwaji Unaoenezwa Kwa Njia ya Mtandao ili Kuwatia Watu Hofu

Taarifa ya Jeshi la Polisi Nchini Kufuatia Upotoshwaji Unaoenezwa Kwa Njia ya Mtandao ili Kuwatia Watu Hofu

Katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la kuwatia hofu wananchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.

Jeshi la Polisi nchini linawataka wote wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote anayo taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze kufanyiwa kazi haraka.

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

 Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.

Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips