Lowassa |
Mchungaji Benedickto Kamzee kutoka Kanisa la Glory of Christ la Katavi amesema wamefikia uamuzi huo wa kuja Dodoma kuonana na Edward Lowassa bila kushinikizwa wala kushawishiwa na mtu yeyote.
“Hakuna aliyetushawishi, hata siyo maaskofu wetu, hili suala halina msukumo wowote zaidi ya msukumo wa Mungu,” alisema Kamzee.
Kamzee alisema wachungaji hao wanatoka kwenye madhehebu ya EAGT, TAG, PEFA, KLPT kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza baada ya kuwakaribisha Wachungaji hao, Lowassa amepinga tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu kwamba amekusanya makundi ya kumuunga mkono huku akidai hana sababu ya kufanya hivyo na hana uwezo wa kuwagharamia watu hao wanao muunga mkono. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment