Mwanamuziki Matonya |
Matonya ameambia Bongo5 kuwa muziki wa sasa hivi upo tafauti na ule wa zamani uliokuwa hauhitaji mambo mengi kama muziki wa sasa.
“Tatizo kubwa kadri siku zinapozidi kwenda wasanii tunazidi kuwa wengi, zamani wasanii walikuwa wanafanya kazi ndogo kwenye muziki wao tofauti na muziki wa sasa ambao kila msanii anataka kuwa juu ya mwenzake,” amesema msanii huyo. “Pia kazi zangu nilikuwa nazisimamia mwenyewe kitu ambacho ilifika wakati hali ikawa ngumu baada ya kushindwa kufanya kila tu. Ila sasa hivi nimejipanga kikamilifu kuna kampuni inaitwa 360 ni ya kwangu lakini nimewapa watu kazi mbalimbali za kusimamia muziki wangu kwahiyo sasa hivi tayari nimeanza kuona utofauti kwenye mapokezi ya ngoma zangu, hii ni dalili kila kitu kitakaa sawa siku za usoni,” ameongeza.
Kwa upande mwingine, Matonya amesema sasa hivi amerudisha mahusiano yake na Tunda Man ambaye walikuwa hawaelewani.
“Tunda hana tatizo na mimi, yule ni mdogo wangu na soon kuna kazi inakuja nikiwa naye, kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula.” WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment