Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Diamond Ajivunia Deal la Milioni 50 Alilopewa Bintiye Tiffah, ni Pamoja na Kuvalishwa Bure na Duka Kubwa la Nguo za Watoto

Diamond Ajivunia Deal la Milioni 50 Alilopewa Bintiye Tiffah, ni Pamoja na Kuvalishwa Bure na Duka Kubwa la Nguo za Watoto

Mtoto wa Diamond Platnumz, Latiffah amepewa endorsement ya shilingi milioni 50 na duka la nguo za watoto ambalo kumvalisha nguo bure ni sehemu ya mkataba huo.


Akiongea jana kwenye hafla iliyoandaliwa na wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete, Diamond alidai kuwa hayo ni sehemu ya maendeleo kwenye muziki yaliyotokea katika mihula miwili ya uongozi wake.

“Katika miaka hii 10 na mtoto nimepata. Mheshimiwa mtoto amezaliwa leo (jana) lakini amepata endorsement leo leo karibuni milioni 50 katika duka tu la kuwa anadhaminiwa kama mtoto anavalishwa na hilo duka, sio maendeleo hayo jamani,?” alihoji Platnumz.

Diamond hakusita pia kuzungumzia rekodi ilivyovunjwa na akaunti ya Instagram ya mwanae, ambayo hadi sasa ina followers zaidi ya elfu 45 siku moja tu baada ya kuzaliwa.

“Katika Afrika ndio mtoto wa kwanza huyo aliyepata followers wengi Afrika nzima, anatokea Tanzania sio maendeleo hayo? WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips