Hii ni Picha iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa Gwajima kafariki dunia na yuko Mochwari.Taarifa hizi zilimpa hofu Gwajima na kumfanya Aagize Bastola yake kwa ajili ya kujihami. |
Utata umeibuka kuhusu bastola waliyodaiwa kukamatwa nayo wafuasi wa Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima baada ya kiongozi huyo kusema anaimiliki kihalali kinyume na maelezo ya polisi.
Gwajima
aliyetolewa kwenye chumba cha uangalizi maalumu cha Hospitali ya TMJ
jana, amelitaka Jeshi la Polisi kurudisha bastola hiyo, akisema ni mali yake na aliiagiza ipelekwe hospitalini kwa sababu ya kujilinda.
Akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo alipolazwa baada ya kuishiwa
nguvu na kupoteza fahamu akiwa katika mahojiano na polisi, Gwajima
alisema anashangaa kukamatwa kwa wachungaji wake waliokuwapo kwa ajili
ya kumlinda.
Hata
hivyo, katika kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema bunduki hiyo haina umiliki halali
wa Gwajima wala wa wachungaji 15 waliokamatwa lakini baadaye jioni baada ya maelezo ya Gwajima, alitoa taarifa akisema bastola hiyo ni mali halali ya askofu huyo. Pia
alisema kuhusu risasi 17 za bunduki aina ya Shortgun, Gwajima anamiliki
bunduki ya aina hiyo lakini akasema uchunguzi kuhusu watu hao 15
unaendelea.
Kauli ya Gwajima
Akizungumza kwa shida akiwa amejishika tumbo, Gwajima alisemaalipopata taarifa za uvumi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia,
aliagiza wachungaji waende hospitalini kwa ajili ya kumlinda, lakini
wakaishia mikononi mwa polisi wakidaiwa kutaka kumtorosha.Kauli ya Gwajima
Alisema
alihofia kuwapo kwa watu wabaya ambao wangeweza kumdhuru halafu
wakasingizia kitendo hicho kufanywa na polisi kwa kuwa alipata tatizo
akiwa mikononi mwao.
“Usiku
wasiwasi ulizidi, huku kila mmoja akiwa hafahamu kwa nini ujumbe wa
namna ile unasambazwa kwenye mitandao, msambazaji ni nani, ana nia gani,
nikaamua kuwaagiza waniletee silaha yangu iliyokuwa kwenye begi ili
likitokea lolote niweze kujilinda,” alisema Gwajima.
Alisema
alishangaa kukamatwa wachungaji wake na kuchukua silaha iliyokuwa ndani
ya begi na hadi jana hakuwa ameulizwa chochote kuhusu umiliki wa silaha
hiyo.
“Kabla
sijazungumza na waandishi kueleza ukweli wa kinachodaiwa kuwa nilitaka
kutoroshwa na wachungaji wangu, nilitaka kuzungumza na ZCO (Mkuu wa
Upelelezi Kanda Maalumu), lakini hajaja, kadi ya ile silaha ninayo,” alisema Gwajima.
Alisema
madai kuwa alitaka kutoroka ilihali polisi alikwenda mwenyewe akitokea
Arusha baada ya kusoma katika vyombo vya habari kuwa anatafutwa.
Alifafanua
kuwa hata alipofika polisi kwa ajili ya mahojiano hakuwa na shaka hata
kidogo, lakini alishangaa kuona anaishiwa nguvu kila baada ya muda na
alipoona kichwa kinamuuma, akawaomba wampeleke hospitali ili mambo
mengine yafuate baadaye, kitu ambacho hakikufanyika kwa wakati.
Wasiwasi kwa polisi
Alisema
alijaribu kuomba apelekwe hospitali mara kadhaa, lakini hakuna
aliyekubaliana naye hadi alipopoteza fahamu na kupelekwa hospitali ya
Polisi Kurasini.
“Hivi
hata kama ni chombo cha usalama, nimepata matatizo nipo mikononi mwao,
halafu nikubali kutibiwa katika hospitali yao, sikulitaka hilo na hata
waliposema nikatibiwe Muhimbili pia sikutaka, ndiyo maana nilikuja hapa,
sisemi moja kwa moja kama Polisi wanahusika lakini kuna vitu vinanitia
shaka,” alisema Gwajima.
Alieleza
kuwa anatilia shaka Jeshi la Polisi kutokana na kuwapo vitu vingi
vinavyoashiria wana kitu kingine wanatafuta, kwani jana tulikuwa na hofu
ya kuvamiwa, waliokuja kutuvamia ni wao, sikugombana na Pengo, nilikuwa
namkemea kama kiongozi mwenzangu wa kiroho wao, wameligeuza ni kesi.
“Sijawahi
kulitilia shaka Jeshi la Polisi lakini katika hili napata wasiwasi
mwingi, sina ugomvi na Kardinali Pengo, nampenda, hajanilaumu, wala
kunishtaki, nilikuwa namkemea katika masuala yetu ya mabaraza ya dini na
siyo vinginevyo,” alisema Gwajima.
Gwajima
pia alionyesha wasiwasi wake kwa kile kilichokuwa kinang’ang’aniwa na
polisi kwenda kupekua nyumbani kwake kuwa hakikuwa kitu kizuri.
Kova alipinga
Wakati
Gwajima akisema hayo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova alisema bastola waliyokutwa nayo wafuasi wa Gwajima
haimilikiwi kihalali.
“Tumegundua
kuwa katika wale watu waliokuwa pale akiwamo Gwajima mwenyewe,
(bastola) haikuwa katika umiliki wao halali, kwa hiyo hapa kuna kesi ya
kupatikana na silaha bila kibali.”
Akizungumzia
tuhuma kwamba polisi walimpekua mke wa Gwajima, Kova alisema hakuna
polisi waliofika nyumbani kwake kufanya upekuzi wowote na kama wakitaka
kufanya hivyo watafuata taratibu maalumu za upekuzi.
Akijibu
swali kuhusu mahali Gwajima alipotakiwa kutoroshewa, Kova alisema
uchunguzi huo bado unaendelea na utakapomalizika wahusika watafikishwa
mahakamani.
Pia alipoulizwa kama Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amemsamehe Gwajima, kwani polisi imng’ang’anie, Kova alisema;“amesema anamsamehe lakini haingilii mambo ya sheria.”
Kuhusu
sababu za Gwajima kuzimia wakati akihojiwa, Kova alisema anayepaswa
kuulizwa kwa nini alianguka wakati akihojiwa na polisi ni Gwajima
mwenyewe.
“Siri
za mahojiano huwa hazitolewi kabla ya ushahidi mahakamani, sababu ya
kupata shock (mshtuko) atajua mwenyewe, kwa kuwa ukifanyiwa jambo
ukafurahi au ukachukia wewe ndiyo unajua ilikuwaje, chochote
kitakachotokea ukicheka, ukinuna, ukizimia, wewe ndiyo tukuulize
ilikuwaje mpaka ukazimia kwa sababu hisia unazipata wewe,”alisema Kova.
Makonda amtembelea
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye alikuwa amemwandikia
Gwajima barua akimwita ofisi kwake, jana mchana alimtembelea hospitalini
hapo kwa ajili ya kumjulia hali kiongozi huyo lakini akasisitiza kuwa
nia yake bado ipo palepale.
“Nilimtaka
leo aripoti ofisini kwangu lakini kwa bahati mbaya anaugua na amelazwa.
Nitakwenda kumuona ili nijue hali yake ikoje,” alisema Makonda kabla ya kufunga safari kwenda hospitali alikolazwa.
Alisema
pia atataka kiongozi huyo wa kiroho amweleze anavyoelewa maana ya uhuru
wa kuabudu unaoelezwa katika Katiba, usajili wa taasisi yake na katiba
ya taasisi hiyo.
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
“Mimi ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni. Niliagiza polisi wamkamate na baadaye wakimaliza kumhoji aje kwangu pia atahojiwa na jopo la watu 20,” alisema Makonda.
0 comments:
Post a Comment