Akizungumza na Clouds Fm, Shyrose alisema kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pumu(asthma) kwa muda mrefu tangu akiwa mdogo lakini safari hii ugonjwa ulizidi sana hali iliomfanya kulazwa hospitali kwa siku kadhaa.
"Huu ugonjwa huwa unanisumbua kwa muda mrefu lakini hadi kufikia hatua ya kulazwa ni safari hii hali ilikuwa mbaya sana lakini namshukuru Mungu nimepewa matibabu naendelea vizuri,’’alisema Shyrose.
Aidha aliongeza kuwa mara ya mwisho kuugua hadi kufikia hatua ya kulazwa ilikuwa miaka mingi sana wakati akisoma nchini Uingereza,pia hali ya hewa ya baridi huwa ni tatizo kwake.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment