Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mwasiti: Napromise March Nitamuweka Boyfriend Wangu kwenye Mtandao ila Sio

Mwasiti: Napromise March Nitamuweka Boyfriend Wangu kwenye Mtandao ila Sio

Baada ya maswali kuwa mengi kuhusu uhusiano baina ya mtangazaji wa EATV/EA Radio, Sam Misago na mwimbaji Mwasiti Almasi, wawili hao wameamua kuzikanusha kwa pamoja taarifa hizo kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV jana Feb 6.

Tarehe 6 Feb. ilikuwa ni birthday ya Sam Misago, na katika kuisheherekea aliwakaribisha studio za EATV wasanii Mwasiti, Damian Soul na Makomando kusheherekea naye mbele ya watazamaji wa kipindi hicho.

Licha ya kuwa Mwasiti alikuwa ameshakanusha siku kadhaa zilizopita kupitia Bongo5 , lakini wawili hao walitumia fursa hiyo wakiwa pamoja kwenye kipindi kukanusha kuwa wao sio wapenzi bali ni marafiki wa takribani miaka sita sasa.

Baada ya zoezi la kukata keki na kulishana kukamilika, Sam alimkaribisha Chitty kuweka sawa taarifa za uhusiano wao. Sam: “Labda Mwasiti anaweza akazungumza na watu akawaambia watu what is going on.”

Naomba niwaambie watu kwamba mimi na Samweli, we are just friends tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sana kwa miaka sita, mi namjua Sam sio vile ambavyo watu wanataka nimjue Sam, mi namjua Sam kivingine, lakini watu wametengeneza mazingira ya kama mpenzi” alisema Mwasiti.

Mwasiti pia alitumia nafasi hiyo kuahidi kumuweka wazi mpenzi wake ifikapo mwezi March mwaka huu.

Mwasiti napromise March ntamweka boyfriend wangu kwenye mtandao, nawaomba kina dada kule msijali mchukueni tu Samweli sio wangu.” Alimaliza

~Bongo5WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips