Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Shemsa Ford. Show all posts
Showing posts with label Shemsa Ford. Show all posts

Siwezi kurudiana na Nay wa Mitego - Shamsa Ford

Ikiwa imepita siku moja toka Nay wa Mitego kupost picha ya Shamsha Ford kwenye mitandao yake ya kijamii ikiwa na ujumbe wa 'Happy Valentine' hususani siku ya wapendanao mwanadada Shamsha Ford amefunguka na kusema

kuwa kamwe hawezi kurudiana kimapenzi na msanii huyo wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Shika Adabu yako'

Shamsha Ford amesema kuwa kwa sasa ana maisha yake na mwanaume mwingine ambaye wanaheshimiana na anampenda hivyo kitendo cha Nay kupost ujumbe wa Valentine akitumia picha yake yeye anaona ni kama msanii huyo anataka kuwakumbusha watu mambo ambayo yeye alishayasahau na mashabiki walisha sahau na kumtaka msanii huyo amuheshimu kwani kwa sasa hayupo kutafuta kiki wala scandal za kijinga.

"Naona mambo yanazidi kuvumishwa kwamba nimerudiana na Nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambae nampenda na kumuheshimu. ..sijarudiana na nay na haiwezi kutokea kabisaaa. ..Nay una ndugu na marafiki wengi wa kuwaposti siku ya leo haikuwa muhimu uniposti mimi. nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na wewe but naona umetaka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA. ..PLS TUESHIMIANE" alimalizia Shamsa Ford
3

Shamsa Ford Na Nay wa Mitego Wakiri Uhusiano Wao wa Kimapenzi

Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford amekiri kuwahi kutoka kimapenzi na Nay wa Mitego na baadaye wakaachana.

Shamsha na Nay wa Mitego walikuwa wakizungumza kwa pamoja ndani ya Global TV hivi karibuni. “Ukweli ni kwamba finally nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Emanuel (Nay) lakini tumeachana,” alisema Shamsa.

Kwa upande wake Nay alisema uhusiano ulikuja baada ya kuwa marafiki.

“Tulikuwa washkaji, mahusiano yetu yalianza hivyo,” alisema rapper huyo.

“Tulienda Masaki baada ya kukaa mida fulani wakati wa kuondoka kusema kweli, kidogo nikaanza kuvutiwa na Shamsa Ford, katika kuagana nikaomba mimi nikamwambia mimi mwenzako matatizo yangu ni haya.

Bahati nzuri yeye pia hakuwa mzito, nahisi na yeye alikuwa amesoma kitu kwangu labda ambacho kilimvutia. Tuli-kiss na for the first time tulikuwa tumeonana siku hiyo na kwamba kila mtu alikuwa tayari kwa lolote litakalotokea. So tukaanza hivyo, kilichotufanya tuendelee kuwa connected ni lile kiss la siku ya kwanza,” aliongeza Nay.3

Shamsa Ford: Natamani Kuolewa na Mtu Ambaye Si Maarufu

Muigizaji wa filamu za Bongo, Shamsa Ford ameweka wazi hisia zake za kutaka kuingia kwenye ndoa.

Shamsa ambaye kwa miezi kadhaa iliyopita amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano na Nay Wa Mitego licha ya kuwepo kwa dalili nyingi zinazoashiria kuwa ni wapenzi, amesema sasa umefika muda anatamani kuolewa.

Muigizaji huyo wa ‘Chausiku’ ambaye ni mama wa mtoto mmoja, ameongeza kuwa licha ya kutamani kuwa mke wa mtu lakini nafasi hiyo hawezi kumpa mtu maarufu, kwa lugha nyingine hawezi kuolewa na Nay Wa mitego.

“Sijui hizi hisia zimetoka wapi…kwa sasa natamani kuolewa na nipo tayari kuolewa ila na mtu ambae si maarufu. Maisha ya usingle nimeshayachoka,” aliandika kupitia akaunti yake ya Instagram.

Wiki mbili zilizopita wawili hao walionekana wakibadilishana mate kwenye birthday ya Shamsa kama inavyoonekana picha hapo juu.
3

Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amemsapoti msanii huyo kwa kuongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya redio na tv ikiwemo Clouds TV na kufanya mahojiano pamoja na kuipush ngoma yake mpya iitwayo Sina Muda.

Akizungumza na Clouds FM,Nay alisema kuwa wamekuwa wakiongozana na Shamsa kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ili kuipa nguvu zaidi na kuitangaza ngoma yake mpya kwa kuwa ni rafiki yake na amekuwa akimsapoti kwenye mambo mengi zaidi ya muziki wake.

‘’Shamsa ni rafiki yangu na amekuwa akinisapoti kwenye mambo mengi tu zaidi ya muziki wangu ndiyo maana nimekuwa nikiongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya TV na redio kwa ajili ya mahojiano na kuitangaza zaidi ngoma yangu mpya ya Sina Muda,’’alisema Nay.

Hata hivyo Nay alisema kuwa ngoma yake hiyo mpya hakuitegemea kama itafanya vizuri kwa kuwa aliichukulia poa na hakuipa nguvu sana lakini ilivyopokewa vizuri na mashabiki ndiyo maana ameona aipe nguvu zaidi kwa kuitangaza kwenye vituo vya redio naTV.

‘’Unajua sikutegemea kama hii ngoma itapokelewa vizuri niichukulia poa tu lakini illivyopokelewa vizuri na mashabiki nimeona bora niipe haki yake nitumie nguvu zaidi kuitangaza nikiwa na binamu yangu Shamsa,’’alisema Nay.
3

Shamsa Ford Aonyesha Jeuri Kumlea Mtoto Wake Bila Msaada wa Baba Yake..Adai Mtoto Hajawahi Kuuliza Baba yake Yupo Wapi

Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonesha jeuri kwa kueleza kwamba anamlea mwanaye Terry kwa mapenzi tele ili asimkumbuke baba yake, Dickson ambaye wamemwagana.

Amesema tangu wamwagane na mzazi mwenzake, mtoto wake hajawahi kumuuliza baba yuko wapi kitendo kinachomfanya azidishe mapenzi kwake kwani hata yeye alilelewa na mama yake bila baba.

  • “Kama baba yake alikuwa akinipiga mbele yake au kuja akiwa amelewa tilalila unafikiri mtoto atamkumbuka? 
  •   
  • Nimelelewa na mama yangu na sikuwahi kumkumbuka baba mpaka hivi nimekuwa mtu mzima, kwa hiyo sioni shida kumlea mwanangu peke yangu, kila kukicha naongeza upendo kwake,” alisema Shamsa.
3

Nay wa Mitego "Shamsa Ford Akitulia Namuhalalisha Kuwa Mke Wangu Kabisa"

Staa wa Bongo Fleva,  Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, ameeleza kuwa endapo staa wa Bongo Movies, Shamsa Ford  ambaye sasa hivi wanapika na kupakua,  atamuonesha utulivu na uaminifu hataona sababu ya kutomuoa.

Nay aliyasema hayo juzikati alipokuwa akizungumzia mipango yake na Shamsa ambaye amejiweka kwake baada ya kutosana na mzazi mwenzake, Siwema. Nay alisema:

 “Hilo la ndoa kiukweli kabisa kama Shamsa ataonesha kutulia na kunithibitishia kuwa hatakuja kunizungua, sitaona hatari kumuoa.”

GPL 3

Shamsa Ford:Mnikome Kuanzia Leo Naishi Nitakavyo Mimi na Kufanya Kile Ambacho Nahic Kinafaida Kwangu

Ustaa kazi: Baada ya kuchoshwa na maneno ya watu kuhusu maisha yake binafsi, staa mrembo wa Bongo Movies, Shamsa Ford ameamua kuweka wazi msimamo wake kwa mashabiki zake wote.

Siku zote nimekuwa muoga kuishi maisha yangu kwa kuogopa watu but hao watu naowaogopa hata siku moja hawajawahi kuogopa kuishi maisha yao kwa kuniogopa mm..from today nitaishi nitakavyo mimi na kufanya kile ambacho nahic kinafaida na kunifurahisha katika maisha yangu.Mashabiki wangu wa ukweli kabisaa alionipangia Mungu hata niweje hawawezi Kunitoka na nitaendelea kuwapenda na kuwaheshimu kila siku..I love my family….” –Shamsa ameandika hayo leo kwenye ukurasa wake mtandaoni. 3

Majirani Wafichua Siri..Kumbe Nay wa Mitego na Mwigizaji Shamsa Ford Wanaishi Nyumba Moja Kama Mke na Mume..Hakuna cha Project Wala nini

Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.

Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili  liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.

Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.

Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:

Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”

Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo 3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips