Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » , » Majirani Wafichua Siri..Kumbe Nay wa Mitego na Mwigizaji Shamsa Ford Wanaishi Nyumba Moja Kama Mke na Mume..Hakuna cha Project Wala nini

Majirani Wafichua Siri..Kumbe Nay wa Mitego na Mwigizaji Shamsa Ford Wanaishi Nyumba Moja Kama Mke na Mume..Hakuna cha Project Wala nini

Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.

Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili  liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.

Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.

Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:

Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”

Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips