1. Kubadili mtindo wa kujikwatua.
Mwanamke anaweza kuwa amezoea kujikwatua kwa namna fulani lakini baada
ya muda akaamua kubadili muonekanao wake kwa kubadilisha aina mpya ya
kujikwatua kwa kuongeza vikorombwezo fulani fulani akitegemea mwenzi
wake ata notes lakini asijue kwamba wanaume kwenye jambo hilo wala
haliwagusi kabisa mpaka wafanye kushtuliwa.
Kwa hiyo nawashauri tu msije mkaumia bure pale mnapoona wenzi wenu hawa notice mabadiliko mliyoyafanya ndivyo tulivyo....
2. Kubadili mtindo wa nywele.
Kwa kawaida wanawake hutumia muda wao mwingi kutengeneza nywele zao ili
kujipa mwonekano mpya na pia wakitarajia kwamba wenzi wao watapenda,
lakini cha kushangaza wenzi wao wala haiwagusi na wala hawa notice
mabadiliko hayo ya nywele mpaka wafanye kushtuliwa na wenzi wao. jambo
hilo huwa linawakwaza sana wanawake, lakini labda tu niwape ushauri wa
bure, msiweke matarajio makubwa ya kudhani kwamba mabadiliko ya nywele
mnayoyafanya yatawavutia wenzi wenu, si kweli utafadhaika bure bora tu
mfanye kwa utashi wenu
3. Kubadili rangi za kucha
Wanaume wengi hawajui tofauti ya rangi, kwa hiyo hata mwanamke abadili
rangi yake ya kucha kwa ajili ya ku match na mavazi fulani aliyonunuliwa
na mwenzi wake au hata aliyonunua mwenyewe anaweza kushangaa mwenzi
wake asishtukie jambo hilo. Ajabu eh!
4. Mkoba mpya.
Unaweza kukuta mwanamke kajinasibu na kununua mkoba mpya wa gharama
baada ya kujinyima sana akitegemea mwenzi wake atauona na kumsifia
lakini atashangaa mwenzi wake wala haulizi anaona tu kama ni mkoba wa
kawaida. Lakini pia hata kama mkoba wenyewe ume match na mavazi bado ni
ngumu kwa mwanaume ku notice na ndiyo maana inawauma sana wanawake
wengi. Mtuhurumie tu, ndivyo tulivyo....
5. Kiatu kipya
Viatu navyo ni eneo lingine ambalo wanaume hawa notice kabisa, mwanamke
anaweza kununua kiatu kipya akitarajia mwenzi wake atakiona na kumsifia
lakini wala, labda tu kama mwanaume huyo anapenda aina hiyo ya kiatu na
aliwahi kukisifia baada ya kumuona mwanamke mwingine amekivaa na
kikampendeza, lakini kama si mpenzi wa viatu wala mwanamke asitarajie
kusifiwa, ni mpaka pale atakapomshtua mwenzi wake kwa kumuuliza kama
kiatu alichovaa kimempendeza au la na sije akashangaa akijibiwa kwa
kifupi tu, "ndiyo" bila comments.
Kwa kawaida wanawake wanapenda ukiwasifia kuhusu jambo fulani utoe na comments japo kidogo tena kwa undani kabisa....
6. Lebasi za ulimbwende na makochokocho mengine
Hereni, bangili na kishaufu au kipini cha puani kinaweza kumpa mwanamke
muonekano mpya, lakini muonekano huo hauwezi kumshangaza mwanaume kama
mwanamke anavyotarajia, jambo hilo huwa linawakera sana wanawake lakini
ukweli ndiyo huo wanaume hawasumbuliwi na vitu vidogo vidogo.
7. Pambo jipya chumbani au kitandani
Mwanamke anaweza kubadili mwonekano wa nyumba au wa chumba cha kulala
akidhani kwamba jambo hilo litamvutia mwenzi wake. si kweli wanaume
hawako hivyo anaweza akafika nyumbani na kuona kama vile hakuna
kilichofanyika mpaka afanye kushtuliwa na mwenzi wake kwa kuulizwa kama
ameionaje nyumba au chumba chao cha kulala. haishangazi mwanaume
akiuliza kwani kuna nini....!
Kwa mwanamke jibu hili anaweza hata kutamani kumtwanga mwanaume na
flower verse kwa hasira, lakini mianaume ndivyo tulivyo, mtuhurumie tu.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment