Klabu ya Manchester United ipo tayari kutoa kiasi cha £25million
kwaajili ya kumsajili Angel Di Maria baada ya winga huyo kukiri anaweza
kuiacha Real Madrid.
Kwa mujibu wa mtandao wa Merto Sport, maafisa wa Old Trafford wamemuweka
Di Maria kuwa miongoni mwa wachezaji wa juu kwenye orodha ya majina ya
wachezaji ambayo wanayafanyia kazi. Pia kwa mujibu wa ripoti za
Hispania, United wapo tayari kutoa £25million na zaidi ili Di Maria
aweze kutua Old Trafford.
Di Maria, ambaye alifunga mabao 11 na kuisaidia Real Madrid msimu
uliopita amesema ana furaha kuendelea kuichezea Real Madri na pia
anaweza kuiacha klabu hiyo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment