Shamsa ambaye kwa miezi kadhaa iliyopita amekuwa akikanusha kuwa na uhusiano na Nay Wa Mitego licha ya kuwepo kwa dalili nyingi zinazoashiria kuwa ni wapenzi, amesema sasa umefika muda anatamani kuolewa.
Muigizaji huyo wa ‘Chausiku’ ambaye ni mama wa mtoto mmoja, ameongeza kuwa licha ya kutamani kuwa mke wa mtu lakini nafasi hiyo hawezi kumpa mtu maarufu, kwa lugha nyingine hawezi kuolewa na Nay Wa mitego.
“Sijui hizi hisia zimetoka wapi…kwa sasa natamani kuolewa na nipo tayari kuolewa ila na mtu ambae si maarufu. Maisha ya usingle nimeshayachoka,” aliandika kupitia akaunti yake ya Instagram.
Wiki mbili zilizopita wawili hao walionekana wakibadilishana mate kwenye birthday ya Shamsa kama inavyoonekana picha hapo juu.
0 comments:
Post a Comment