Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Lulu: Ifike muda tutumie mitandao ya kijamii kusaidiana mawazo na sio kutukanana

Lulu: Ifike muda tutumie mitandao ya kijamii kusaidiana mawazo na sio kutukanana

Moja ya mambo sita tuliyoandika kuwa ni sababu ya watanzania kuupenda mtandao wa Instagram, ni kushuhudia matusi ambayo mastaa wanayavuna kutoka kwa followers wao.

Lakini unadhani Instagram inapaswa kuwa sehemu ya kihuni kiasi hicho? Hapana.

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael anaamini hawezi kufikia malengo yake kwa mawazo yake pekee bali anahitaji msaada kutoka kwa vijana wenzake ambao nao wana nia na malengo kama yake katika kufikia ndoto zao. Ndio maana anahisi Instagram inaweza kuwa ni sehemu nzuri ya vijana kupenda michongo na sio matusi.

Nikiwa Kama Kijana Mpenda Maendeleo, mwenye ndoto na malengo ya kufika mbali najua mawazo yangu peke yangu yanaweza yasitoshe mimi kufika ninapopataka,” ameandika kwenye Instagram.

Najua wapo vijana wengi wenye nia kama yangu..!Nadhani umefika wakati wa kutumia mitandao ya kijamii Kwa kujengana na kusaidiana hasa ki mawazo Ili wote tuweze Kuwa sehemu fulani siku moja.”

Lulu ameonesha wazi kuwa hapendezwi na tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya hasa kwa kudhalilishana.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips