Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe amesema kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.
Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu baada ya kuwa rais kwa miaka 10.
Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi na kukimbilia nchini Tanzania.
Hata hivyo umoja wa Afrika mashariki unadaiwa kushindwa kutoa amri dhidi ya Rais Nurunziza kutokana na kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani kinyume na katiba ya nchi hiyo suala linalopingwa vikali na wananchi wa nchi hiyo.
Tanzania Hottest Celebrity Gossip News WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment