LULU MICHAEL |
Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka na yupo ‘flati skriini’.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.
- “Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.
Baadaye alitumiwa ujumbe wa kwanza uliosomeka: “Tafadhali naomba upokee simu, nahitaji kuzungumza na wewe jambo muhimu.” Hata hivyo, hakujibu.Baada ya kuona kimya, mwandishi wetu alimtumia ujumbe ulioonesha madai hayo: “Kuna tetesi kuwa ulinasa mimba na kuficha na sasa inadaiwa kutoka na kwamba hata chuoni haukuwa ukihudhuria, hili likoje?”
Baada ya kimya cha saa kadhaa, Lulu alijibu:
- “Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.
Gallos Official Blog
Tanzania Hottest Celebrity Gossip News
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment