Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

Shamsa amsapoti Nay Wa Mitego kui’push’ ngoma yake mpya ya ‘Sina Muda’.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego amemsapoti msanii huyo kwa kuongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya redio na tv ikiwemo Clouds TV na kufanya mahojiano pamoja na kuipush ngoma yake mpya iitwayo Sina Muda.

Akizungumza na Clouds FM,Nay alisema kuwa wamekuwa wakiongozana na Shamsa kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ili kuipa nguvu zaidi na kuitangaza ngoma yake mpya kwa kuwa ni rafiki yake na amekuwa akimsapoti kwenye mambo mengi zaidi ya muziki wake.

‘’Shamsa ni rafiki yangu na amekuwa akinisapoti kwenye mambo mengi tu zaidi ya muziki wangu ndiyo maana nimekuwa nikiongozana naye kwenye vituo mbalimbali vya TV na redio kwa ajili ya mahojiano na kuitangaza zaidi ngoma yangu mpya ya Sina Muda,’’alisema Nay.

Hata hivyo Nay alisema kuwa ngoma yake hiyo mpya hakuitegemea kama itafanya vizuri kwa kuwa aliichukulia poa na hakuipa nguvu sana lakini ilivyopokewa vizuri na mashabiki ndiyo maana ameona aipe nguvu zaidi kwa kuitangaza kwenye vituo vya redio naTV.

‘’Unajua sikutegemea kama hii ngoma itapokelewa vizuri niichukulia poa tu lakini illivyopokelewa vizuri na mashabiki nimeona bora niipe haki yake nitumie nguvu zaidi kuitangaza nikiwa na binamu yangu Shamsa,’’alisema Nay.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips