Nchemba aliomba radhi bungeni jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM) kuomba muongozo, akihoji sababu za Serikali kushindwa kupeleka fedha hizo vyuoni.
“Mheshimiwa Spika, naomba nipewe mwongozo ni kwa sababu gani serikali imeshindwa kupeleka fedha huku ikijua wazi kwamba wanafunzi hao ni watoto wa masikini,
Katika taarifa yake, Nchemba alisema kutokana na kuchelewa huko aliwaomba radhi wanafunzi ambao wanasoma kwa kutegemea mkopo wa serikali huku akizitaka mamlaka husika kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanafunzi mara moja. Alisema Hazina imekwisha kuidhinisha fedha hizo.
“Juzi hazina ilikamilisha miamala ya fedha ambazo zinahitajika katika vyuo hivyo na mamlaka zinazohusika zilipaswa kufikisha fedha hizo jana kwa wahusika (wanafunzi),” alisema Nchemba na kuongeza:
“Ni muda mrefu migomo haijatokea kutokana na ukweli kuwa mtiririko wa utoaji wa fedha haukuwa na matatizo.
“Hakuna hata wa kulikuza suala hili kwa sababu msingi wake ulikuwa ni wa halali lakini kwa sasa limepatiwa ufumbuzi,” alisisitiza.
Kuchelewa kutolewa fedha hizo za mkopo kumesababisha wanafunzi wa vyuo hivyo kugoma kuanzia juzi hadi watakapopewa fedha hizo za kujikimu.
Bulaya katika taarifa yake alisema wanafunzi zaidi 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) juzi waligoma kuingia darasani kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu huku wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilicho Mbezi, Dar es Saam wakisimamishwa masomo.
Mwisho WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment