Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo
wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka
madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa
cha Usafirishaji (NIT)
Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana
kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.
Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.
Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment