Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts

CCM Yawatupia Lawama Wakurugenzi Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar ......Yadai Wanawahujumu ili UKAWA Washinde

Wakati waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tamisemi na utawala bora George Simbachawene akitoa muda wa uchaguzi wa mameya kukamilika ifikapo machi 25 mwaka huu,Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba “Gadafi” amemuomba Waziri  huyo kuangalia upya  utendaji kazi wa wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni, akidai wamevuruga uchaguzi wa meya na naibu wake.

Akizungumza na wanahabari jana, Simba alisema CCM imefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa wakurugenzi hao, ikiwamo kushindwa kutafsiri vyema vifungu vya sheria vilivyosababisha kuondolewa kwa majina ya wajumbe wao kwa madai kuwa hawana sifa za kushiriki uchaguzi huo.

“Wakurugenzi hawakuwa majasiri katika kupambana na vitisho vya wajumbe wa Ukawa na kuwa wakweli. Walishindwa kutoa tafsiri sahihi ya wajumbe halali wanaotakiwa kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa jiji,” alilalamika Gadafi.

Kwenye mkutano huo Gadafi alidai kwamba wakurugenzi hao walifanya upotoshaji wa tafsiri sahihi kuhusu uwepo wa wajumbe wa CCM walioonekana kutokuwa wajumbe halali.

“CCM imesikitishwa na upotoshaji uliofanywa na wakurugenzi hao hasa kwa kuwavua uhalali wa kupiga kura baadhi ya wajumbe wetu,” alisemea na kuongeza;

“Wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni wamekula matapishi yao, haiwezekani uchaguzi wa awali wawakubali wabunge viti maalum kama wajumbe halafu uchaguzi wa jiji waseme hawastahili kupiga kura.”

Gaddafi alidai kwamba, Ukawa ndio walikuwa wa kwanza kuuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa walitumia njia ya vitisho na kuwafanya wakurugenzi wafanye maamuzi kulingana na mashinikizo yao.

Alidai kwamba, licha ya CCM kuonekana kuwa chanzo cha kuvuruga uchaguzi huo lakini chama hicho hakina sababu hata moja ya kufanya hivyo isipokuwa ni utaratibu wanaoshinikiza ufuatwe na kuwa wana mgombea bora na anayekubalika.

“Wajumbe wa Ukawa ndiyo walianza kukiuka taratibu za upigaji kura kwa kupiga picha kura walizopiga na kumuonesha mmoja kati ya viongozi wao.

“Uchaguzi hupigwa kwa siri, iweje Ukawa wawalazimishe wajumbe wao kupiga picha kura walizopiga? Ina maana wanaogopa wajumbe wao wasije wakaipigia kura CCM,”alisema. 3

Naipongeza Rasmi UKAWA Mpaka Hapa ilipofikia...Naiona CCM Kama Chama cha Upinzani Miaka Ijayo

Kwakweli kwa mtanzania anayefikiri kwa kina ataungana na mimi kwamba, pamoja na hujuma na figisufigisu nyingi zilizofanyika ambazo ziko wazi japo ukweli hausemwagi Tanzania, UKAWA kwakweli wameimarisha upinzani.

Ninachokiona mimi ni CCM kuwa chama cha kawaida cha upinzani siku za usoni.. Sasa hii itawezekanaje? Twende pamoja nitoe yangu ya moyoni

1. Niwakati sasa wakutambua kwamba kwakuunganisha nguvu ndo dawa pekee itakayosaidia kummaliza mtawala CCM. Kwa hili naomba niseme viongozi wa UKAWA zitambueni fitna zinazotimiwa na CCM kuwachonganisha na kuwagawa, naomba muwe werevu muwazidi akili zaidi shikamaneni.

2. Hakikisheni mnapigania kwa udi na uvumba kupatikana kwa katiba mpya yenye dira na muelekeo sahihi, itakayoweza kusema fulani kashinda mpeni haki yake,

3. Jikiteni Sasa kutoa elimu vijijini ambao wengin kwasababu hawazijui changamoto kali za maisha na wengine wakiamini kuwa CCM ni ile ile ya nyerere y ujamaa basi wa
naipa kura tu,

4. Dumisheni Democrasia kwa vyama vyote vya "UKAWA" viwe na haki sawa ya kutangazwa na kuimarishwa,

5. Tofauti na chama tawala nyie wekeni uwazi wa kila kitu kinachofanyika ili kuongeza imani za wafuasi

6. La mwisho kwa sasa, dumisheni kwa pamoja na kwa uhalisia kumtegemea Mungu aliyeumba majira na nyakati.

By H.T. 3

CCM, Kuipoteza Dar es Salaam ni Kuipoteza Tanzania Nzima

Dar es Saaam ndiyo Tanzania. Dar es Salaam ndiyo kila kitu. Kioo cha Tanzania ni Dar es Salaam. Pamoja na uwepo wa majiji matano nchini: Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Tanga, lakini Dar ndiyo mwanzo na mwisho. Katika uchaguzi huu, CCM imenyanyasika vya kutosha Dar.

Kati ya majimbo kumi, saba yamenyakuliwa na wapinzani. Matatu tu ndiyo yako chini ya CCM. Kabla ya uchaguzi huu, Dar ilikuwa na majimbo saba. Wapinzani walikuwa na mawili tu. Mambo yamebadilika.

Hii inamaanisha kuwa Manispaa za Dar es Salaam zitaongozwa na wapinzani. Kwahiyo, ni kama kusema, Serikali ya Dar es Salaam itakuwa ni Serikali ya wapinzani. CCM imepokwa uongozi wake hapa Dar es Salaam. Ni jambo zito. Ni jambo la maumivu makali.

Hata vigogo wa nchi hii wanaendelea kuishi kwenye jimbo linaloongozwa na wapinzani: Kawe. Vyuo vikuu karibu vyote vya Dar es Salaam vipo Kinondoni yenye majimbo manne: Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba. Yote yamenyakuliwa na upinzani. Yaani, Dar es Salaam ipo chini ya utawala wa UKAWA.

Sauti iliyovuma kutoka Arusha hadi Mbeya; toka Mbeya hadi Mara; toka Mara sasa imetua Dar es Salaam. Yote yafanyike lakini hili la Dar linauma sana. Ndiyo maana hata mpambano wa Urais bado ni mbichi sana kwakuwa majimbo ya Dar es Salaam bado hayajatangazwa.

Kuna la kufanyika kichama mwaka 2020!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam 3

Orodha ya Majimbo ambayo CCM Wameyapoteza Mpaka Sasa

1.Monduli
2.Simanjiro
3.Same Mashariki(Mama Kilango)
4.Siha
5.Bunda Mjini(kwa Wasira)
6.Arumeru Magharibi-hili Jimbo bado liko CCM
7.Jimbo la Christopher Chiza(huko mkoa wa Kigoma)
8.Tanga Mjini
9.Babati Mjini
10.Babati vijijini
11.Tandahimba
12.Muleba kusini(sina uhakika sana)
13.Moshi vijijini
14.Tunduma
15.Mtwara mjini
16.Bukoba Mjini(confirmed)
17.Tarime vijijini(John Heche kashinda)
18.Tarime mjini
19.Mwanga(sina uhakika sana).
20.Serengeti
21.Sengerema
22.Kaliua
23.Ndanda
25.Kigoma mjini
26.Rorya
27.Ukonga

Morogoro tumechukua majimbo mawili nitayaongeza soon.


Orodha inaendelea,ongeza na mengine niliyoyasahau.

By by Salary Slip/JF
Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney Advertisement3

CCM Wailalamikia tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)

Na Mhamed khamis Zanzibar. 
Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar kimesema hakina imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uendeshaji nzima wa uchaguzi. 
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa Naibu katibu mkuu CCM Bwana Vua Ali Vuai amesema baadhi ya maeneo mawakala wa Chama chao walinyimwa vitamulisho jambo ambalo limekifanya chama hicho kutokuridhika na utaratibu huo. 
Amesema siku moja kabla ya uchaguzi walifika tume ya uchaguzi kuhakiki vitambulisho vya mawakala wao wote na vilikuwepo. 
Amesema cha kushangaza ni kuwa siku ya kura vitambulisho vya mawakala hao havikuonekana wala hakujulikana nani alivichukua
"Kutokana na hali hii tunakosa imani na ZEC " alisema Vuai.
ANGALIA VIDEO HAPA:


Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney 3

Yaliyojiri Mkutano wa CCM na Waandishi wa Habari, Ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Dar 16 Sept 2015


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tumewaita kuwaomba mtusaidie kufikisha ujumbe ufuatao kwa Watanzania:

MWENENDO WA KAMPENI ZA CCM

Hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.


Kwa upande wa kampeni zetu za Ubunge, zaidi ya robo tatu ya wagombea Ubunge wa CCM wamekwishazindua kampeni zao na wanaendelea vizuri. Sekretarieti ya Kampeni ya CCM inaanda program maalum ya kampeni katika majimbo yenye changamoto mahsusi.

Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wana-CCM kwamba viongozi na makada wengine wa CCM, waliopo madarakani na wastaafu watapita tena, jimbo kwa jimbo, nchi nzima katika siku 30 za mwisho katika jitihada za kuongeza ushindi wa CCM na Dr. Magufuli.

MIDAHALO YA WAGOMBEA

Wiki tatu zilizopita, CCM, na kwa hakika vyama vingine pia, ilipokea mwaliko wa Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Urais uliondaliwa na Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza. Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo. Kwa msingi huo, kauli ya UKAWA iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndugu James Mbatia, kwamba UKAWA inaomba mdahalo ni njia ya kuwahadaa Watanzania tu kwa kuwa mwaliko wa mdahalo ulikwishatolewa mapema kwa vyama vyote na wanaotakiwa kushiriki ni wagombea Urais wa vyama.

CCM inafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza katika chaguzi zetu. Na inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais ni
sehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni.

Hatukubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Tunaamini hoja hii ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao. Tunaamini mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea. Wao ndio wanaoomba dhamana. Wao ndio wanaopaswa kujibu maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao.

CCM inaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana
kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki.

UCHAGUZI WA AMANI

CCM inasikitishwa na kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA zenye kuashiria fujo na vurugu. Kauli kwamba kura zitaibiwa hazina msingi wowote. Kauli hizi zinaashiria maandalizi ya kushindwa na maandalizi ya kufanya vurugu baada ya matokeo ya kushindwa.

Utaratibu wa uchaguzi wetu unajulikana na umekubalika na vyama vyote. Kura zinapigwa kituoni na kuhesabiwa kituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Baada ya kura kuhesabiwa, matokeo yanajazwa katika fomu ambayo kila wakala anasaini na kupewa nakala. Nakala ya matokeo hayo pia inabandikwa nje ya kituo cha kupiga kura. Kila Chama, na kila Mtanzania, kina fursa ya kujumlisha matokeo yake kwenye kila kituo na kupata jumla kuu. Matokeo ya nchi nzima yanajumlishwa mahala pamoja huku kukiwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wawakilishi wa vyama vyote na wao wakiwa na fomu zao za kila kituo nchi nzima.

Tunapenda kuwasihi Watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu. Mara nyingi, viongozi wanaohamasisha vurugu wanakuwa na ulinzi au walinzi au uwezo wa kukimbilia pahala penye utulivu zaidi huku wakiwaacha wafuasi wao katika wakihangaika.

UCHAGUZI NA UMOJA WA KITAIFA

CCM pia inapenda kusisitiza imani yake kwamba uchaguzi haupaswi kutugawa kama taifa. Uchaguzi ni tukio la kupita. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Kuna taifa baada ya uchaguzi. Lazima taifa liendelee kubaki moja, tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli za kupitiliza zenye mrengo wa kujenga chuki katika jamii na kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Kama Chama kilichoasisi umoja wa taifa letu, tunaendelea kuasa kwamba wanasiasa wasijinadi kwa misingi ya udini, ukabila wala ukanda. CCM haina mpango kuendeleza mjadala wa kauli ya Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa aliyoitoa kanisani Tabora tarehe 6 September 2015
kwamba nchi ilishapata viongozi Wakatoliki na kwamba sasa ni zamu ya Walutheri kuchukua nafasi hiyo. Tunaamini mjadala huo hauna tija. Tunaamini kwamba Watanzania wengi, wa dini na madhehebu yote, hawaamini katika siasa za namna hii. Tuliamini kwamba UKAWA ingetumia fursa ya mkutano wao na waandishi wa habari jana kuomba radhi kwa Watanzania. Kwakuwa hawakufanya hivyo, tunapendekeza mjadala wa jambo hili ufungwe. Itoshe tu kwamba Ndugu Lowassa amesema hivyo, Tume ya Uchaguzi imemuonya, na yeye hajajitokeza kuomba radhi wala kufafanua. Watanzania wamemjua ni kiongozi wa aina gani na watatoa hukumu yao tarehe 25 Oktoba 2015.

Imetolewa na:-

January Y. Makamba,

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI YA CCM
16/9/2015
3

CCM Kuzidisha Muda wa Kampeni, NEC Waitupia Mpira Polisi

Sarakasi zinaendelea.Tume ya uchaguzi NEC imenukuliwa ikiwatupia mpira jeshi la polisi kuwa ndilo linalohusika kuhakikisha kampeni hazizidi saa 12.Tume imeruka kimanga baada ya kupokea hoja kutoka kwa wadau kuwa juzi CCM wakati wakizindua kampeni Jangwani walizidisha muda zaidi ya nusa saa kinyume na taratibu... 3

Mambo 20 ya Kushangaza Niliyojifunza Kwenye Mkutano wa CCM Jagwani Haya Hapa....


1. Yamoto Band wameshangiliwa zaidi kuliko Magufuli

2. Wakati Mbowe amewakutanisha Lowasa na Sumaye. Leo Jakaya amewakutanisha Diamond na Ali Kiba Jangwani,

3. CCM wanajua kuwa mikutano ya UKAWA inapata mafuriko, kwa hiyo nao walijitahidi wapate "mafuriko"

4. Watu wengi wameenda kuwashangaa wasanii, sio kumsikiliza Magufuli. Kumuona Diamond bei ghali, leo wamemuona Live bila kiingilio wataacha kwenda?

5. Magufuli anajua lugha nyingi za makabila kuliko anavyojua matatizo ya wananchi,

6. Mkapa anahitaji maombi ya kufunga maana anazeeka vibaya. Amemuita Mpumbavu, Waziri Mkuu aliyemteua mwenyewe na kufanya nae kazi miaka 10,

7. Mwisho wa mikutano ya siasa ni saa 12 kamili lakini CCM wamezidisha dakika hadi 12:40. Ikiwa wameshindwa kutekeleza Sheria waliyoiweka mwenyewe, watawezaje kutekeleza ahadi zao? CCM hawapaswi kuaminiwa,

8. Kitendo cha Magufuli kukiri serikali inanyanyasa Machinga na mama Ntilie ni kukiri kuwa serikali yake imechoka na inahitaji kubadilishwa,

9. Magufuli amemvua nguo Kikwete hadharani. Kusema anashangaa meno ya tembo yamefikaje uarabuni ni kusema kuwa JK anashiriki biashara hiyo. Ikiwa Magufuli amesema atazuia biashara hiyo haramu, nini kimemshinda JK kuzuia kwa sasa?

10. Magufuli anajua kuwa CCM inakaribia kufa. Wakati akimalizia hotuba yake ametoa mfano ambao haukueleweka vizuri, lakini fundisho lake ni kuwa WATANZANIA MSIIUE CCM. Kumbe anajua kuwa CCM itakufa,

11. Ccm wamewadharau sana watanzania kwa kuwapandisha malori ya kubebea vitunguu, nyanya na viazi. Mtanzania aliyepandishwa lori leo akiipigia kura CCM atadhihirisha kuwa yeye ni kiazi,

12. Mzee Warioba ameshindwa kabisa kumnadi Magufuli kwa hoja. Kwa namna alivyojieleza anaweza kuzidiwa na kijana aliyemaliza form four akapata division zero,

13. Mzee Mkapa ana matusi "makali" kuliko wafanyakazi wa bar,

14. Bila msaada wa malori na kujazia bodaboda mafuta, uwanja wa Jangwani leo ungekua mtupu,

15. Warioba anaipenda CCM zaidi ya anavyoipenda Tanzania,

16. Rais Kikwete amekiri kuwa Magufuli alikua chaguo lake, it means hakuwa chaguo la wanaCCM. Kwa lugha rahisi Kikwete amedhihirisha kuwa alienda Dodoma akiwa na majina yake mfukoni kama ilivyodaiwa,

17. Kwa kuwa Polepole alikiri Warioba ni "Role Model" wake, leo tumemjua anayemtuma Polepole kutukana UKAWA,

18. Jeshi la Polisi linatumika kisiasa. Wameshindwa kuzuia maandamano "haramu" ya CCM na kuzuia mkutano ilipofika saa 12 kamili kama sheria inavyotaka,

19. Miongoni mwa watu wanaopaswa kuchunguzwa UKAWA ikishika dola ni pamoja na Jaji Joseph Warioba na Mzee Mkapa,

20. CCM haifai kuendelea kuwa madarakani baada ya October 25.

By G Eng Ole Philemon 3

CCM Yatangaza Kamati ya Kampeni za Uchaguzi Yenye Watu 32 Chini ya Abdulrahman Kinana

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa juzi Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

1.    Ndugu Abdulrahman Kinana        -    Mwenyekiti
2.    Ndugu Rajab Luhwavi     -    Makamu Mwenyekiti – Bara
3.    Ndugu Vuai Ali Vuai      -     Makamu Mwenyekiti - Z’bar
4.    Ndugu Sofia Simba
5.    Ndugu Mohamed Seif Khatib
6.    Ndugu Asha-Rose Migiro
7.    Ndugu Samwel Sitta
8.    Ndugu Nape Nnauye
9.    Ndugu Mwigulu Nchemba
10.    Ndugu Harrison Mwakyembe
11.    Ndugu January Makamba
12.    Ndugu Amina Makillagi
13.    Ndugu Christopher Ole Sendeka
14.    Ndugu Stephen Wasira
15.    Ndugu Abdallah Bulembo
16.    Ndugu Hadija Aboud
17.    Ndugu Mohamed Aboud
18.    Ndugu Lazaro Nyalandu
19.    Ndugu Issa Haji Ussi
20.    Ndugu Waride Bakari Jabu
21.    Ndugu Mahmoud Thabit Kombo
22.    Ndugu Shamsi Vuai Nahodha
23.    Ndugu Maua Daftari
24.    Ndugu Stephen Masele
25.    Ndugu Pindi Chana
26.    Ndugu Shaka Shaka
27.    Ndugu Makongoro Nyerere
28.    Ndugu Bernard Membe
29.    Ndugu Sadifa Juma Khamis
30.    Ndugu Antony Diallo
31.    Ndugu Livingston Lusinde
32 .    Ndugu Ummy Mwalimu3

CCM Wayapuuza MAFURIKO ya Lowassa......Nape Asema Hata Mrema Alikuwa Kivutio. Ataka Gari la WAGONJWA Lipelekwe Kwa Lowassa Mapema

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza kuwa kitashinda Uchaguzi Mkuu mwaka huu kwa sababu kina mtandao mkubwa wa wanachama kuanzia ngazi ya chini na kwamba kufurika kwa wananchi katika mikutano ya Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa sio ushindi, kikisema kura ni mahesabu.

Aidha, kimesema kuwa mgombea huyo wa Chadema na umoja wa vyama vinne vya upinzani (Ukawa), amedanganywa na wapambe wake kuihama CCM na kumkejeli ikisema gari la wagonjwa linapaswa kuwekwa nyumbani kwake siku ya uchaguzi kwani CCM itapata ushindi wa uhakika asubuhi.

Akitoa taarifa kuhusu kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika jana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisisitiza kuwa ushindi wa chama hicho tawala na kikongwe hauna shaka kutokana na mtandao wake kuanzia ngazi ya chini.

Akijibu swali kuhusu kufurika kwa wananchi katika mikutano ya mgombea huyo wa Chadema, Nape alisema:

“Kwa walioanza siasa jana ndio watashituka. Mwaka 2010 Slaa (Dk Willibrod) katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni Mbeya alipata watu wengi kuliko wale aliopata Edward. Lakini kura alizopata Mbeya utashangaa.

“Kupata watu wengi mkutanoni hakutushangazi kwani kura ni mahesabu, hawa (Chadema na mgombea wao) wanatoka pointi moja kwenda nyingine. CCM ina mtandao, ukiondoka mjumbe wa nyumba kumi anapitia watu wake anasafisha nyayo zenu,” alisema kiongozi huyo.

Nape aliongeza kuwa wapinzani wote wametoka ndani ya CCM kuanzia kwa Augustino Mrema mwaka 1995 na hadi katika chaguzi nyingine zilizofuta na zote wapinzani walishindwa, na hata safari hii CCM itashinda.

Akimgeukia Lowassa, Nape alisema Waziri Mkuu huyo aliyejiuzulu, amedanganywa na wapambe wake na kuondoka chama tawala, na kwamba licha ya kuhamia huko, CCM itamshinda asubuhi na kuwataka wanaotishia kukihama kufanya hivyo na si kuleta shinikizo.

“Katika mchakato wa uchaguzi si wote watakaoridhika na matokeo kwa sababu kuna wengi wanajiandaa kushinda na sio kushindwa, na matokeo yanapokuwa hivyo, wanakuwa hawaridhiki na hapo ndipo wanazungumzia kwenda upande wa pili, na hasa kwa shinikizo la wapambe.

“Hili limetokea kwa Edward, amekwenda upande wa pili, amedanganywa na watu, tutampiga. Ushindi wa CCM ni wa uhakika, sio wa matumaini. Matumaini yapo Angaza, CCM ni ya uhakika. Tutashinda asubuhi. Tumesema ni mpambano kati ya wagombea na makapi,” alisema Nape na kuongeza:

“Zipo mechi ambazo unajua hii utashinda. Yanga na Lipuli ya Iringa unajua matokeo yake. Tunataka mgombea mwenzetu apelekewe ambulance (gari la wagonjwa) nyumbani kwake, kwani ushindi kwetu ni uhakika.

” Kuhusu wanaolalamika na kutishia kuhama, alisema malalamiko hayawezi kutolewa barabarani kwani chama hicho kina utaratibu wake na yale yote yaliyolalamikiwa yakiwamo ya udiwani, yamefanyiwa kazi.

 “Tulisema wakati ule wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kuwa hatutafanya kazi kwa shinikizo. Tunajua uimara wa chama chetu, kama kuna watu wanataka kwenda upande wa pili waende. Lakini CCM haiwezi kufanya kazi kwa vitisho na shinikizo.

"Tatizo ni kwamba kunatokea wagombea 12, halafu unasema lazima uwe wewe. Kuna watu (wanaotaka kuhama) wanafanya hivyo kwa shinikizo la viroba na hela,” alisema Nape. 3

CCM Wakanusha Habari Iliyoenea Kuwa Mgombea Wake, Dr John Magufuli Ameahidi Kugawa Laptop Kwa Walimu Wote Nchini

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha uvumi ulioenea sehemu mbalimbali kuwa Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chama hicho,Dkt.John Pombe Magufuli amewaahidi Walimu kuwapa Kompyuta kama CCM itapita madarakani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema kauli hiyo siyo ya kweli na haikutolewa na Mgombea huyo wa Urais,Dkt.Magufuli.

Hatahivyo,Nape amesema kauli hiyo imetolewa kwa nia mbaya kuonyesha Chama cha Mapinduzi kimeanza ziara ya kampeni mapema.

Amesema watu walioinukuu kauli hiyo wamesema imetoka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho.

" Ilani ya Uchaguzi ya CCM imetoka juzi Agosti 13,2015 katika Mkutano wa Chama uliofanyika juzi mjini Dodoma na inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 23 mwaka huu katika uzinduzi wa Kampeni,hivyo kauli yoyote iliyotoka kwa chama hicho ikidaiwa imetoka katika Ilani yetu ya Uchaguzihiyo siyo ya kweli,kwani Ilani hiyo itazinduliwa wakati wa uzinduzi wa kampeni Agosti 23" alisema na Nape kwa msisitizo.

Kuhusu msimamo wa Chama cha Mapinduzi kwa wanachama wanaohama chama hicho,Nape amesema wanachama hao wanahama kwa mapenzi yao binafsi wengine wamehama kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni za chama.3

Majina Rasmi ya Wagombea Ubunge CCM 2015 Yatajwa-Anna Tibaijuka na Job Ndugai Ndani

Majina ya walioteuliwa kugombea ubunge wa majimbo na uwakilishi wa viti maalum kupitia CCM katika majimbo yote Tanzania yametoka rasmi , yupo Iddi Azzan anagombea Jimbo la Kinondoni, Prof. Anna Tibaijuka anagombea jimbo la Muleba Kusini.
Nape Nnauye anagombea jimbo la Mtama., Nimrod Mkono anagombea jimbo la Butiama, Ndugu Ridhiwani Kikwete anagombea Chalinze na Job Ndugai ameteuliwa kugombea Kongwa.

Kujua wote walioteuliwa kuwakilisha majimbo na viti maalum Bonyeza Link Hii Hapa chini:





Attachment: 

3

Mabalozi Mia Moja wa CCM Monduli, Wahamia CHADEMA

Mabalozi wa mashina miamoja na kumi wa CCM mwenyekiti katibu kata wajumbe wa kamati ya siasa ya kata pamoja na wenyeviti wa mitaa minne katika kata ya Monduli mjini mkoa Arusha wamehama CCM na kuhamia Chadema.

Tukio ilo limetokea Monduli mjini leo majira ya saa sita mchana wakati viongozi hao walipo kusanyika na kutoa kauli ya kuhama CCM na kuhamia Chadema huku wakieleza sababu zinazo wafanya kufikia maamuzi hayo.

Kwa upande wao wenyeviti wa serikali za mitaa wajumbe wa nyumba kumi na katibu wa CCM kata ya Monduli Anna Erinest wameitaka jamii itambue kuwa hayo ni maamuzi yao binafsi na hayahusiki na shinikizo la mtu yoyote kama inavyo daiwa na baadhi ya watu kila wanaohama udaiwa wameshinikizwa. 3

Madiwani 18 wa CCM Wahamia CHADEMA

Madiwani 18 wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametangaza kuhama chama hicho jana jijini Arusha.

Madiwani hao waliotangaza kuihama CCM walikuwa katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Arumeru.

Huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias Ngorisa aliyefuatana na Diwani wa Kata ya Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo, ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro naye pia amejiunga na Chadema.

Walikuwepo wazee wa mila wa Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka Engusero Sambu. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na kuwapatia kadi za Chadema.

Akizungumza baada ya kupokea kadi, Elias Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya 28 ambao tayari wamechukua kadi za Chadema na kuondoka CCM na watatetea nafasi zao kupitia Chadema katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

Alisema yapo mabadiliko makubwa na Watanzania hawana budi kuyakubali na ameshawishika kubadilisha mwelekeo toka CCM kwenda Chadema.

Kwa upande wake, Diwani Ngukwo, alisema, amekihama chama hicho kwa sababu anahitaji mabadiliko na anaamini wengi watawafuata ili waweze kuondokana na manyanyaso mengi ya Loliondo wanayopata. 3

Kura za Maoni CCM: Mawaziri Watano Waanguka.......Yumo Chikawe,Sillima,Mahanga na Makalla.......Aden Rage Pia Kaanguka!!

Matokeo ya awali ya kura za maoni kwa wagombea udiwani na ubunge kupitia chama tawala, yameanza kuanikwa, huku yakionesha kuwa baadhi ya mawaziri, wabunge na watendaji katika chama na serikali wameangushwa.


Kwa mujibu wa matokeo ambayo mtandao huu umeyapata, kwa upande wa mawaziri walioshindwa ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

 Hayo yamethibitishwa na Katibu wa CCM mkoa wa Lindi, Adelina Gefi aliyesema kura za Chikawe katika jimbo lake la Nachingwea alikokuwa anatetea kiti chake, hazikutosha mbele ya Hassan Masalla, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero aliyepata kura 6,444. Chikawe amepata kura 5,128.

Wakati Chikawe, mmoja wa wanasiasa mahiri na mwanasheria aliyepata kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora na pia Waziri wa Katiba na Sheria akikwama katika mchakato wa kurejea bungeni, naibu wake katika Wizara wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima naye ameanguka katika kura za maoni huko jimbo la Bumbwini, Unguja.

Mwanasiasa mwingine aliyekwama katika kura za maoni ni Mahadhi Juma Mahadhi ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mahadhi ameanguka katika kura za maoni katika Jimbo la Paje, Unguja huku mshindi akiibuka kuwa Jaffar Sanya Jussa.

Mambo yamekuwa mabaya pia kwa Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima ambaye ameripotiwa kuanguka katika kura za maoni katija Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani.

Hali kama hiyo imemkuta Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Milton Makongoro Mahanga ambaye ndani ya saa 24 tangu ashindwe kura za maoni katika jimbo alilokuwa analitumikia la Segerea katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, jana alitangaza kuihama CCM na kujiunga na Chadema.

Katika Jimbo la Mvomero mkoani Morogoro, habari zinasema aliyewahi kuwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Suleiman Saddiq `Murad’ amefanikiwa kumwangusha mshindani wake wa siku nyingi, Amos Makalla ambaye alilitwaa jimbo hilo mwaka 2010 na baadaye kuteuliwa kuwa Naibu Waziri, akianzia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Maji ambako yupo mpaka sasa.

Ingawa Katibu wa CCM wa wilaya ya Mvomero, Amos Shimba hakuthibitisha hilo, akisema kwa kiasi kikubwa matokeo yamepatikana, isipokuwa katika baadhi ya maeneo, hivyo matokeo rasmi yatatangazwa leo, tayari kambi za Murad na Makalla zilithibitisha matokeo ya kura za maoni katika jimbo hilo, kwamba hali ya Makalla haikuwa nzuri katika kura hizo.

Mshtuko mwingine wa kisiasa umesikika katika Jimbo la Uzini ambako mwanasiasa nguli aliyepata kuwa waziri katika wizara mbalimbali za Serikali ya Muungano, Muhammed Seif Khatib ameshindwa katika kura za maoni.

Khatib ambaye kwa sasa ni Katibu wa Oganaizesheni ya CCM, amepata kura 1,333 dhidi ya mpinzani wake, Salum Mwinyi Rehani aliyepata kura 1,521.

Khatib amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20 na katika kipindi hicho alikuwa waziri wa wizara mbalimbali zikiwemo Habari na ile ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Rage `out’, Adadi, Nape safi
Ukiachilia mbali mawaziri hao, baadhi ya wabunge wamekuwa na wakati mgumu majimboni kwao, akiwemo Ismail Aden Rage wa Tabora Mjini. Aidha, Zainabu Kawawa, binti wa Waziri Mkuu wa zamani, Rashid Mfaume Kawawa hakufua dafu mbele ya Mbunge wa Jimbo la Liwale, Faith Mitambo.

Awali, Zainabu alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya CCM.

Mbunge mwingine aliyeshindwa katika kura za maoni ni Mtutura Abdalla wa Tunduru Kusini, kama ilivyokuwa kwa wabunge watatu wa mkoa wa Tanga, Herbert Mntanga wa Jimbo la Muheza aliyeangushwa na Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI).

Saleh Pamba, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Maliasili ambaye anamalizia ubunge wake katika Jimbo la Pangani, amethibitika kukwama mbele ya Jumaa Awesso, kwa mujibu wa Katibu wa CCM mkoa wa Tanga, Shija Othman.

Mbunge wa Korogwe Mjini, Yussuf Nasri naye kura zake hazikutosha, baada ya wanachama wa CCM kumpa kura nyingi Mary Chatanda kuwa ndiye chaguo lao katika kura za maoni ya ubunge.

Naye Gregory Teu, Mbunge wa Mpwapwa aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, ameripotiwa kuanguka na mbunge wa zamani wa Jimbo hilo, George Malima Lubeleje.

Katia Jimbo la Kilombero, Abdul Mteketa amegota mbele ya Abubakar Asenga, wakati katika Jimbo la Igalula mkoani Tabora, Naibu Waziri wa zamani wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba anaburuzana na Mussa Ntimizi, ambapo kufikia jana Ntimizi alikuwa na zaidi ya kura 75,000 dhidi ya 3,400 za Mfutakamba.

Kibamba ni Dk Mukangara
Kwa upande wa baadhi ya majimbo ya Dar es Salaam, walioshinda kwa upande wa CCM ni pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara aliyeshinda kura za maoni katika jimbo jipya la Kibamba lililogawanywa kutoka jimbo la Ubungo, huku Ramesh Patel aking’ara Jimbo la Ukonga alikowabwaga washindani kadhaa, akiwemo Meya wa Manispaa wa Ilala, Jerry Silaa.

Katika jimbo la Ubungo, kura zimempa nafasi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, wakati Abbas Mtemvu ameshinda katika jimbo la Temeke analoliongoza tangu mwaka 2005.

Nape apeta Mtama
Nako katika Jimbo la Mtama lililoongozwa kwa miaka 15 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kabla ya mwaka huu kujitosa katika mbio za urais, kijiti kinaelekea kumwangukia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliyewabwaga washindani wake kadhaa, akiwemo Suleiman Mathew aliyekuwa Diwani wa Kata ya Vijibweni, Kigamboni 3

Wagombea Ubunge Tarime Wakamatwa Kwa Kutengeneza Kura FEKI

Uchaguzi wa kura za maoni kupitia CCM katika jimbo la Tarime Mjini na Vijijini umeahirishwa hadi kesho baada ya kukamatwa makaratasi maalum ya kupigia kura (kura feki ) zaidi ya elfu 20 zikiwa na majina ya wagombea, Nyambare Nyangwine na Gaudencia Kabaka yakiwa tayari yameshawekewa alama ya NDIO kuonesha kura zimekubaliwa
3

CCM Wataja Sababu Kadhaa Kwanini Jina la Lowassa Lilikatwa Mchakato wa Mgombea Urais CCM..Nimekuweka Hapa Sababu Hizo

Ndugu wananchama wa Chama cha Mapinduzi-CCM ni wiki mbili tangu tulipo maliza mchakato ndani ya chamakumpata mgombea wa Urais hapo octoba 25,2015. Kwa mara ya kwanza wananchama 41 waliomba kuteuliwa na chama. Hii inaonyesha kwamba demokrasia imekuwa ndani ya chama. Kati ya wanachama wa CCM waliochukua fomu alikuwa ni mheshimiwa waziri mkuu mstaafu Ndugu Edward Lowasa. Utaratibu wa chama ulifuatwa ili kumpata mgombea ikiwa ni pamoja kamati ya maadili, kamati kuu na halmashauri kuu ya taifa na mkutano mkuu. Katika mchakato pia chama kilitumia idara mbalimbali kama usalama wa taifa, takukuru na tume ya maadili ya umma kupata taarifa mbalimbali kuhusu wagombea hasa za uadirifu, usalama wan nchi na kadhalika.

Baada ya mchakato kumalizika baadhi ya wagombea na wanachama hawakuridhika na matokea, katika chama kikubwa kama CCM haiwezekani wanachama wote wakaridhika na maamzi. Ndugu wanachama na watanzania tunaomba kuelewa kuwa kumpata kiongozi mkubwa wa nchi kama Rais siyo kazi rahisi. Baadhi ya wanachama ambao hawakuridhika na maamzi ya chama ni Ndugu Edward Lowasa, amekuwa akizungumza nje ya chama kuhusu kutotendewa haki na baade kuhama chama na kujiunga na chamacha demokrasia na maendeleo-CHADEMA.

Kwa nini Ndugu Lowasa hakuteuliwa kuwa mgombea wa CCM?
Ndugu wanachama na watanzania, Mheshimiwa Lowasa alijenga hisia na kuamini kuwa ndani ya CCM wagombea wote walistahili kuenguliwa isipokuwa yeye. Hii siyo demokrasia, baada ya kupitia repoti mbalimbali Ndugu LOWASA alienguliwa kwa sababu zifuatazo:-

1.Kukiuka taratibu za chama kwaani alionekana kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini

2.Kutoa rushwa kwa wanachama mbalimbali hivyo kukigawa chama na kama angepishwa kuwa mgombea CCM ilikuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi mahakamani lakini pia angeweka watu wake kwenye utawala kuwalipa fadhira.

3.Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC uliofanyika miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC.

4.Kuanza kampeni kabla ya wakati, alikuwa akisafirisha watu mbalimbali na kuwalipa fedha nyingi kisha kutoa taarifa kuwa walikuwa wakimtaka kugombea Urais, hii ni hadaa na hatari kwa chama

5.Kuwa na kashfa nyingi za ufisadi3

VIDEO:Mheshimiwa Ndugai Amechimbia Kaburi la Kisiasa Baada ya Kumshambulia Mgombea Mwenzake Kwa Gongo Mpaka Kuzimia...

Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa. Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

 Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye Ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi.. Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu. Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia
"Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

 Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi.. Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio...

Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika. Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada ya kupata PF 3 toka polis

VIDEO HII HAPA:
3

CCM Kumjibu LOWASSA Leo

Baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kutangaza kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na kuhamia Chadema jana katika ukumbi wa Bahari Beachi jijini Dar es salaam, chama cha Mapinduzi kimetoa taarifa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari  leo.

Taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi haijafafanua kuwa ajenda itakuwa nini katika kikao hicho lakini kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujibu shutuma zilizotolewa na Lowassa kuhusiana na madai ya kuwepo uonevu wakati akiomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM.

Mtandao huu utakujulisha kitakachojiri katika mkutano huo 3

Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo

Chama  cha  mapinduzi, CCM kimemteua  Dr .Magufuli  kuwa  mgombea  wa  Urais  2015.
Uteuzi wa  Dr. Magufuli  umetokana na  ushindi  wa  kishindo  alioupata  baada  ya  mkutano  mkuu  kukutana jana   usiku  kwa  ajili  ya  kupiga  kura  ili  kupata  jina moja  kati  ya  matatu  yaliyokuwa  yamependekezwa  na  Halmashauri  kuu  ya  CCM.
 Matokeo  ni  kama  ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%
3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips