Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar kimesema hakina imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uendeshaji nzima wa uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa Naibu katibu mkuu CCM
Bwana Vua Ali Vuai amesema baadhi ya maeneo mawakala wa Chama chao
walinyimwa vitamulisho jambo ambalo limekifanya chama hicho
kutokuridhika na utaratibu huo.
Amesema siku moja kabla ya uchaguzi walifika tume ya uchaguzi kuhakiki vitambulisho vya mawakala wao wote na vilikuwepo.
Amesema cha kushangaza ni kuwa siku ya kura vitambulisho vya mawakala hao havikuonekana wala hakujulikana nani alivichukua
"Kutokana na hali hii tunakosa imani na ZEC " alisema Vuai.
ANGALIA VIDEO HAPA:Quote: What we have, what we wish we had - ambitions fulfilled, ambitions disappointed, investments won, investments lost, elections won, elections lost - these things may occupy our attention, but they do not define us. By Mitt Romney WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment