Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mabula Ashinda Ubunge Jimbo la Nyamagana..Amgaragaza Vibaya Ezekiel Wenje

Mabula Ashinda Ubunge Jimbo la Nyamagana..Amgaragaza Vibaya Ezekiel Wenje

By Louis Kolumbia/Sauli Giliard Mwananchi Digital
Dar es Salaam.  Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stanslaus Mabula ametangazwa mshindi wa mbio za ubunge katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza kwa kupata kura 81, 170 dhidi ya mbunge anayemaliza muda wake, Ezekiel Wenje (Chadema) aliyepata kura 79, 280.

Akitangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Nyamagana, Peter Mainya, amesema jumla ya wagombea saba walichuana kuwania nafsi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa Nyamagana.

Mainya amesema, ushindi wa Mabula umetokana na msingi uliowekwa na chama chake katika matokeo ya uchaguzi wa udiwani ambapo kati ya Kata 18 zinazounda jimbo hilo, CCM imeweza kujinyakulia Kata 14 huku Kata nne zikichukuliwa na Chadema.

“Kutokana na msingi huo, Stanslaus Mabula ameweza kupata kura 81,170. Hivyo basi, kwa mamlaka niliyopewa, namtangaza Stanslaus Mabula kuwa ndiye mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Nyamagana” alisema Peter Mainya.

Ezekiel Wenje anakuwa mbunge wa pili wa upinzani kupoteza kiti chake jijini Mwanza baada ya Highness Kiwia aliyekuwa anatetea kiti chake cha ubunge katika  jimbo la Ilemela kuangushwa na Anjela Mabula katika matokeo yanayoashiria kurejea kwa utawala wa CCM katika siasa za Mwanza.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips