Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo
yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua
ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.
Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua
gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini,
kutokana na kile kilichoelezwa
kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni
kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni
Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam
na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo
wabunge.
Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia
ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na
Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake, aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.
“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali
sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia,
aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua
nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.
Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine,
hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa
mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye
alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo,
haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati
wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....
0 comments:
Post a Comment