Taarifa zilizopatikana jana usiku na kutangazwa na Shirika
la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo
anahojiwa kuwapo kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo
mwanafunzi wala mtumishi katika chuo hicho.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa
watu wanne waliokuwa wamejificha katika mabweni ya chuo hicho na kati
yao, wawili walibainika kuwa ni wanafunzi.
Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba
alipoulizwa jana kuhusu Mtanzania huyo, alisema atatoa taarifa rasmi kwa
taratibu za jeshi hilo.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment