Jane Matinde kutoka Airtel anakwambia ishu nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa kupitia chanel ya TRACE URBAN ambayo ni namba 325 kwenye DSTV Jumamosi hii tarehe 18 April 2015.
Ni shindano ambalo lilihusisha washiriki walioanza kwa kupiga simu kuonyesha uwezo wao na kurekodi moja kwa moja ambapo jamaa wamekuja kufanya hesabu na kukuta simu zilizopigwa ni jumla ya milioni mbili na laki tatu na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na Marekani kama vile ya voice na idols.
Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015 ambapo Jumamosi watazamaji na majaji watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa Marekani ambapo kwa pamoja ni dili lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/= ambapo ni zaidi ya 920000000 za kibongo.
Show itaonekana Jumamosi hii saa tatu usiku na kurudiwa Jumapili tarehe 19 kuanzia saa kumi jioni hapohapo TRACE URBAN ikiwa ni show itakayochukua dakika 90.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment