Familia za wanafunzi 142 kati ya 148 waliouawa katika shambulio la kigaidi la Al Shabaab kwenye Chuo cha Garissa Kenya
wameruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao kwa ajili ya mazishi ambapo
Serikali ililazimika kutumia mashine maalum kutambua baadhi ya miili
ambayo iliharibika vibaya kutokana na majeraha ya risasi.
Hilo limeendelea lakini bado kuna ishu
oinawaacha watu njia panda, zaidi ya wanafunzi 166 hawajulikani walipo,
familia zao bado zimeendelea kulalamika kutokana na baadhi ya ndugu zao
kutoonekana.
Uamuzi mwiingine mgumu uliotangazwa na
Kenya ni kulitaka Shirika la Wakimbizi UNHCR ndani ya miezi mitatu
kufunga kambi ya wakimbizi iliyoko mashariki mwa nchini hiyo pamoja na
kuwarudisha kwao wakimbizi ambao ni raia wa Somalia zaidi ya laki nne.
Bonyeza play kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment