Katika cheche zake hizo, mtaalamu huyo wa masuala ya rushwa na ufisadi, ataweka hadharani majina ya vigogo na makada wa chama waliokuwa wakimchimba mkwara na kuwaachia wafanye yao ili kulinda kibarua chake tukufu.
Katika orodha hiyo ya Dr Hosea wamo watu wazito kutoka serikalini waliokuwa wakimuandikia vimemo mara kwa mara wakati wanapopitisha makontena yao bila kulipia ushuru na kuikosesha serikali mabilioni ya shilingi za mapato.
Aidha, inasakikiwa kwamba kwenye orodha pia wamo wauza unga na majangili wakubwa waliokuwa wakipitisha unga na vipusa mtawalia, kupitia banadari ya Dar es Salaam bila kuguswa na mtu yeyote. Pia wamo vigogo waliomshika mikono wakati anashugulikia skandali ya EPA, ESCROW na nyinginezo.
Mtakumbuka kwamba kuna kada mmoja wa ngazi ya juu anayetajwatajwa sana kuhusika katika biashara haramu ya meno ya tembo ambaye meno hayo yalipatikana yamepakiwa kwenye meli yake siku za nyuma yakiwa yamesafirishwa hadi nchi za mbali.
MAONI YANGU
Magufuli jiandae kwenda mbali zaidi kushughulikia waliotoa vimemo, kwa muktadha huo utakuwa umeiteketeza CCM nzima kuanzia juu mpaka chini.
Source:Jamii ForumsWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment