Taarifa za ndani ya Stanbic zinadai kuwa benki hiyo imeshindwa kutaja
majina ya waliochota mabilioni ya Escrow kwa Malumbesa na Rambo. Taarifa
hizo zinadai kuwa, pamoja na kuwepo kwa nia hiyo, benki hiyo ilikumbana
na vikwazo vya ndani na nje ya benki hiyo hadi kukubali kukaa kimya.
Ilipangwa kuwa,majina ya waliochota mabilioni ya Escrow kupitia miamala
ya Stanbic yangewekwa hadharani hadi kufikia Aprili 1,2015.
Hatahivyo, Stanbic inadaiwa kuwatimua kazi wafanyakazi mbalimbali
waliohusishwa na miamala hiyo iliyokuwa na harufu na tuhuma za ufisadi.
Wafanyakazi hao ni wa ngazi na kada mbalimbali ndani ya Stanbic. Huu
ndiyo mwisho wa filamu ya kujulikana kwa waliochota mabilioni ya Escrow
kwa lumbesa na rambo? Tujipe moyo!
By Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es SalaamWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment