Kati ya majimbo kumi, saba yamenyakuliwa na wapinzani. Matatu tu ndiyo yako chini ya CCM. Kabla ya uchaguzi huu, Dar ilikuwa na majimbo saba. Wapinzani walikuwa na mawili tu. Mambo yamebadilika.
Hii inamaanisha kuwa Manispaa za Dar es Salaam zitaongozwa na wapinzani. Kwahiyo, ni kama kusema, Serikali ya Dar es Salaam itakuwa ni Serikali ya wapinzani. CCM imepokwa uongozi wake hapa Dar es Salaam. Ni jambo zito. Ni jambo la maumivu makali.
Hata vigogo wa nchi hii wanaendelea kuishi kwenye jimbo linaloongozwa na wapinzani: Kawe. Vyuo vikuu karibu vyote vya Dar es Salaam vipo Kinondoni yenye majimbo manne: Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba. Yote yamenyakuliwa na upinzani. Yaani, Dar es Salaam ipo chini ya utawala wa UKAWA.
Sauti iliyovuma kutoka Arusha hadi Mbeya; toka Mbeya hadi Mara; toka Mara sasa imetua Dar es Salaam. Yote yafanyike lakini hili la Dar linauma sana. Ndiyo maana hata mpambano wa Urais bado ni mbichi sana kwakuwa majimbo ya Dar es Salaam bado hayajatangazwa.
Kuna la kufanyika kichama mwaka 2020!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment