Stephen Wassira |
Wassira amedai kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.
Ester Bulaya Aliyemwangusha Wassira |
Alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye matokeo hayo na kwamba tarakimu hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuzidi idadi iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia amedai kuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo bila kuzingatia sheria ya uchaguzi.
Ester Bulaya na Wassira ni mahasimu wakubwa wa kisiasa ambao walianza ushindani mkubwa katika jimbo hilo tangu Ester Bulaya alipokuwa mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment