Agness Masogange |
Akizungumza na gazeti hili, Masogange alimlaumu Diva, kwa kitendo chake cha kuandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram kuwa alizungumza na Davido ambaye alikana kuwa na uhusiano na msichana yeyote kutoka Tanzania.
“Kinachonishangaza kwanini Diva afikie hatua ya kumpigia mpaka Davido kumuuliza kuhusu uhusiano wangu na mwanamuziki huyo, kitu ambacho kimeshangaza hata msanii mwenyewe,”alisema Masogange.
Diva Loveness wa Clouds FM |
Masogange alionesha kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram meseji alizokuwa akimtumia mwanamuziki huyo, akishangazwa na dhamira ya swali hilo.“Inawezekana Diva anatafuta kiki kupitia jina langu, maana kila mtu anagombana naye, sasa huyo ni mtu wa aina gani jamani,” alisema Diva.
Diva, mmoja kati ya wanahabari wenye jina kubwa, alitafutwa kupitia simu yake ya kiganjani, lakini kwa muda mwingi iliita bila kupokelewa.
GPL WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment