Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Updates:Askari Polisi Wanne Wamejeruhiwa katika Mapambano na Magaidi Tanga.

Updates:Askari Polisi Wanne Wamejeruhiwa katika Mapambano na Magaidi Tanga.


Hadi sasa taarifa kutoka mkoani Tanga zinaeleza kuwa askari wanne wa Jeshi la Polisi Tanzania wamejeruhiwa katika mapambano dhidi ya vikundi vya kihalifu (kigaidi) katika eneo machimbo ya Amboni mkoani humo.
Taarifa zaidi zinasema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga kwa matibabu zaidi na kuna watu wawili ambao wamekamatwa kuanzia jana hadi sasa wakihusishwa na tukio hilo.

Aidha, mmoja wa Askari waliopo katika eneo la tukio amesema mapema leo asubuhi Helkopta ya Polisi ilinusurika kudunguliwa na vikundi hivyo vinavyosadikiwa kuwa viko zaidi ya vinne.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa kila kona ya eneo hilo imeelezwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani Tanga atatoa taarifa ya tukio hilo saa 15:00pm.

UPDATES II:
Pango walimojificha magaidi limevunjwa kwa kutumia mizinga, na hatimae jamaa wametoroka hakuna aliekamatwa, Sergeant Kajembe wa JWTZ aliepigwa risasi ya Tumbo ameshafariki Dunia, majeruhi waliopo hospital ni PC mmoja wa FFU, Sergeant wa JWTZ aliejeruhiwa sikio, Corporal alijeruhiwa mguu.

Askari wote wameshatawanyika eneo la Tukio na walichokuta ni Pikipiki, baiskeli, vyakula na nguo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips