Madiwani hao waliotangaza kuihama CCM walikuwa katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilayani Arumeru.
Huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elias Ngorisa aliyefuatana na Diwani wa Kata ya Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo, ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro naye pia amejiunga na Chadema.
Walikuwepo wazee wa mila wa Kabila la Wamasai (malaigwanani) Laurence Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka Engusero Sambu. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, ndiye aliyewapokea makada hao na kuwapatia kadi za Chadema.
Akizungumza baada ya kupokea kadi, Elias Ngorisa, alisema wapo madiwani 18 kati ya 28 ambao tayari wamechukua kadi za Chadema na kuondoka CCM na watatetea nafasi zao kupitia Chadema katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.
Alisema yapo mabadiliko makubwa na Watanzania hawana budi kuyakubali na ameshawishika kubadilisha mwelekeo toka CCM kwenda Chadema.
Kwa upande wake, Diwani Ngukwo, alisema, amekihama chama hicho kwa sababu anahitaji mabadiliko na anaamini wengi watawafuata ili waweze kuondokana na manyanyaso mengi ya Loliondo wanayopata. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment