Baada ya kuvuja kwa video ikionyesha jinsi rapper Jay Z akipigwa na
shemeji yake (Solange) wakiwa kwenye lift huku Beyonce mwenyewe akiwa
pembeni yao akishuhudia ugomvi bila kujihusisha wala kuzuia, uongozi wa
hoteli ugomvi huo ulipotokea huko New York umesema unachunguza kujua
video hiyo ilivuja vipi na kupeleka siri za wateja kwenye vyombo vya
habari.
Kwenye ugomvi huu ambao Jay Z ameonekana kusifiwa na watu wengi kwa kuwa
mkimya na bila kujibu mashambulizi pamoja na kupigwa mateke na
kurushiwa vitu, tayari watundu wa mitandaoni wameanza yao kwa
kutengeneza picha na maandishi vikimtania Jay Z pamoja na Solange.
Kutokana
na ile single ya Jay Z iitwayo ’99 problems’ yaani matatizo 99… watu
wamemtengenezea utani kwamba Solange ni tatizo la 100 la Jay Z.
Sehemu
ya utani mwingine ni hii ya historia kwenye wikipedia ya Solange na
kuifanya itoe maelezo kwamba Solange ni mwimbaji, mwandishi wa nyimbo,
kicker, streetfighter na tatizo la 100 la Jay Z.
0 comments:
Post a Comment