Msanii wa Bongefleva ambaye jina lake lilianza kushine kwenye game ya muziki wa Bongofleva toka akiwa na umri mdogo Mr. Blue, amerudi kwenye headlines baada ya kupost kupitia account yake ya instagram na kuelezea hisia zake kuhusu wimbo mpya alioutoa Mr. II Sugu kuwa ni wimbo ambao alimshirikisha na anashangaa kuona mambo yapo tofauti.
Katika post ya instagram Mr. Blue aliandika “Ndugu
zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana
kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia
..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa
makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa
wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na
kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake
tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je
hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au
sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu
zangu….????”
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment