Kwani Floyd Mayweather kafilisika?
kaamua kuususa mkanda wake? au ndio mwendelezo wa zile mbwembwe zake?
Kweli kaamua kuuachia mkanda wake hivihivi kisa deni la Mil 446?
Story ya mwishomwisho kusikika kuhusu
yeye ilihusu Shirikisho la Ngumi Duniani WBO kutangaza kumvua mkanda
alioshinda baada ya kumpiga Manny Pacquiao kutokana na deni la Dola 200,000 (ni kama Tshs. 446) ambazo ilitakiwa alipie kama kodi baada ya pambano lake na Manny Pacquiao!!
Tukiachana na stori hizo najua kuna
mastory mengi kuhusu jamaa kustaafu, maswali kuhusu nani atapanda nae
jukwaani hivi karibuni.. ninayo hii list ya Mabondia ambao wametajwa
kwamba huenda mmoja wao akapanda kuzipiga nae kabla hajastaafu.
Kiukweli kwenye hii list hakuna mwenye rekodi mbaya, kila mmoja ni mkali yani.
Wakati utafika na tutajua tu nani
atakutana ulingoni na mbabe huyu wa karne, swali ni kwamba atakubali
rekodi yake ya ushindi wa mapambano 48 iharibike?
0 comments:
Post a Comment