Zimebaki kama wiki mbili hivi ugeni wa
White House utue pale Jomo Kenyatta International Airport, Nairobi Kenya
kama ambavyo iliahidiwa.
Safari ya kihistoria ya Rais Obama
ndani ya Kenya inakaribia, huu ni uthibitisho mwingine kwamba mambo
yameiva… Gari za watu wa Usalama tayari zimeshushwa Nairobi na pia kuna
Helicopter zaidi ya nane za Kijeshi tayari zimetua.
Mbali na gari hizo pamoja
na helicopter zilizotua, wako Maofisa Usalama zaidi ya 200 ambao tayari
wako Kenya kwa ajili ya kuhakikisha mpaka siku Rais Obama anatua kunakuwa na usalama wa kutosha.
Stori nyingine kutoka Nairobi inaonesha
timu ya watu wa Usalama watakuwa kama 800 hivi kutoka Marekani na Polisi
zaidi ya 2,000 wa Kenya watahusika na Ulinzi wa msafara wa Obama akiwa
Kenya.
0 comments:
Post a Comment