BIASHARA ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao
vikao vya kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
vimekwisha kuanza.
Uchunguzi uliofanywa katika baadhi ya kumbi kama Club
Maisha, Club Laazizi na Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo
idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.
Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo
hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja
bila ya wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema wako kibiashara
na siyo kuuza sura.
Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku
kucha akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea
magari huku wakitafuta wateja wenye magari.
Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema,‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?
‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume na wanatoa ‘mpunga’ nadhani huyu rais ajaye atakuwa na neema.’’
Dada mwingine ambaye aliyekuwa Dodoma Carnival karibu na
Kituo Kikuu cha Mabasi, alisema ametoka Arusha akiwa na marafiki zake
kwa lengo la kuwafuata wateja wa msimu walioko Dodoma.
Alisema hadi sasa ana siku tatu akiwa Dodoma na tayari
amekusanya zaidi ya Sh 700,000 huku akiwatumia madalali ambao
huwaunganisha kwa wateja
0 comments:
Post a Comment