Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mzee Yusuph kuoa tena mke wa watatu,Wake zake watupiana vijembe mtandaoni

Mzee Yusuph kuoa tena mke wa watatu,Wake zake watupiana vijembe mtandaoni


Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni.

Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani.

Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.

Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.

‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,"alisema Mzee Yusuph. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips