List
ya makocha wa mpira wa miguu wanaoongoza kwa kulipwa vizuri kwenye soka
mpaka sasa ambapo namba 1 imechukuliwa na Pep kama unavyoona list nzima
hapa chini
1. Pep Guardiola
Huyu ni kocha wa Bayern Munich,
ameitumikia timu yake kwa mafanikio makubwa huk akiisaidia kupata
mataji mbalimbali, ndiye kocha anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa
kuliko wote kwa kupokea kiasi cha dola milioni 24
2. Jose Maourinho
Huyu ni kocha wa Chelsea ambaye
anajulikana kwa kuwa na maneno mengi,kwa sasa yupo mbioni kuwania
ubingwa wa ligi kuu ya England, ni kocha anashika nafasi ya pili kwa
kulipwa kiasi kikubwa cha pesa na hupokea kiasi cha dola milioni 17.
3. Marcello Lippi
Ana mchango mkubwa kwenye Timu ya Taifa ya Italy na kufanikiwa kutwaa kombe la dunia mwaka 2006, anapokea kiasi cha dola milioni 14.
4. Fabio Capello
Huyu ni kocha wa timu ya Taifa ya Russia, anapokea kiasi cha dola milioni 13
5. Carlo Ancelotti
Huyu ni kocha mkuu wa Real Madrid, anapokea kiasi cha dola milioni 10.5.
6. Arsene Wenger
Amekuwa kocha wa Arsenal toka mwaka 1996, na anapokea kiasi cha dola milioni 10.
7. Gerardo Martino
Huyu ni kocha wa Argentina, anapokea kiasi cha dola milioni 7.5.
8. Jurgen Klopp
Huyu ni kocha wa Borrusia Dortmund, anapokea kiasi cha dola milioni 6.
9. Manuel Pellegrini
Huyu ni kocha wa Manchester City, anapokea kiasi cha dola milioni 5.75.
10. Jorge Jesus
Huyu ni kocha wa klabu ya Benefica tangu mwaka 2009, anapokea kiasi cha dola milioni 5.5
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment