Watu
wanaoishi Njoro Kaunti ya Nakuru, Kenya wameiomba Serikali ya nchi hiyo
kuwasaidia eneo la kufanyia mazishi kutokana na uhaba wa ardhi.
Ishu ni kwamba kutokana na maeneo ya
makaburi kutotosha watu wamejikuta wakilazimika kuchimba makaburi yenye
vina vifupi juu ya makaburi mengine ili waweze kufanya mazishi.
“Serikali
itupatie mahali ambapo tunaweza kuzika watu wetu kwa amani.. sio
ukizika ukienda kulima unapata umefufua mtu mwingine… mnarudi mnamuweka
pembeni hata yeye hilo kaburi lilinunuliwa ilipaswa na yeye aweze
kuzikwa”– alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.
Ukosefu wa ardhi ya kuzikia ni taatizo kubwa linalokumba maeneo mengi nchini humo.
Nimekuwea sauti ya taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…
0 comments:
Post a Comment