Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mahabusu Afia Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki baada ya Kujitundika na Kunyinyonga

Mahabusu Afia Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki baada ya Kujitundika na Kunyinyonga


Picha si ya Tukio hilo
Mahabusu mmoja Shabani Ramadhani (28), amekutwa amejinyonga katika choo cha Kituo cha Polisi Ubungo- Urafiki, jijini Dar es Salaam.



Tukio hilo lilitokea jana baada ya mahabusu huyo kufikishwa katika kituo hicho juzi akituhumiwa kufanya tukio la unyang’anyi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Augustino Senga, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa marehemu alijinyonga kwa kutumia kamba ya kaptura aliyovaa.

Kamanda Senga alisema marehemu alijinyonga alfajiri katika choo wanachokitumia mahabusu hao na mwili wake kugundulika nusu saa baadaye.

“Alikwenda chooni kati ya majira ya saa tisa na saa kumi alfajiri wakati wenzake wakiwa wamelala na ndiko alikojinyongea kwa kutumia kamba ya kaptura yake, lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Senga.

Mama mdogo wa marehemu ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema kuwa  Ramadhani alikamatwa na Polisi Ijumaa iliyopita na kufikishwa katika kituo hicho akiwa salama.

Alisema jana walifika katika kituo hicho kwa ajili ya taratibu za kumwekea dhamana, ndipo walipoelezwa kuwa ndugu yao amefariki dunia kwa kujinyonga na kamba.

“Sisi wenyewe tunashangaa iweje kajinyonga wakati tunavyofahamu mtuhumiwa anapofikishwa polisi anatolewa vitu vyote alivyonavyo na kuingizwa mahabusu?,” alihoji mama huyo.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips