Majina ya maofisa hao yamepelekwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili wachukuliwe hatua.
Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa ameambiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (Taa), George Sambuli kuwa maofisa hao wameondolewa uwanjani hapo.
Sambuli amesema: “Wale watumishi waliokuwapo pale tulichukua hatua za awali za kuwahamisha,pia tuliandika taarifa na kuipeleka wizarani tunasubiri maelekezo zaidi.”
Awali, maofisa hao walitoa majibu yanayotofautiana kuhusu mashine ya ukaguzi iliyopo kitengo cha ukaguzi wa mizigo.
Amesema wamejitahidi kushughulikia wizi wa mafuta ya ndege uliokuwapo katika maeneo ambayo hayakuwa na kamera baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua hatua.
Profesa Mbalawa amesema taarifa hiyo haijamfikia mezani kwake kwa kuwa alikuwa katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.
“Tumeamua kufanya ziara na Katibu wa Wizara ili kuona maelekezo aliyotoa Rais, tumeona mashine zote zinafanya kazi, lakini tunaangalia mafanikio na changamoto ambazo wanakabiliana nazo,” amesema WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment