May 23 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wawili wa serikali, taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo imeeleza kuwa Rais wa Magufuli amemteua Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya
Uteuzi huo, Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri
(Cabinet Clerk), Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tulia Ackson
ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi. Kabla
ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi
katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na uteuzi huu umeanza mara moja.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment